Kutokana na somo hili linalohusu je Shetani anaweza kuzuia maombi? Majibu swali hilo tunawe kuyapata kwa njia ya neno la Mungu ambalo ndio kweli. Ukweli wa neno la Mungu ndio njia sahihi kwa ajili ya kuthibitisha mambo yote. Kwa sababu hiyo yatupasa kuthibitisha mambo yote ambayo tunaamini kama ni sahihi na neno la Mungu. Jinsi ya kufahamu mambo yale tunayoamini kama ni sahihi ni pale yanapokuwa yanaendana au kukubaliana na neno la Mungu. Hiyo ndio imani sahihi. Lakini ikiwa mambo yoyote tunayoamini yanapingana na neno la Mungu hiyo ni imani isiyo sahihi. Kwa sababu hiyo mtu anakuwa anaishi kinyume na neno la Mungu. Ni muhimu kufahamu ya kwamba mtu ambaye anaishi katika imani isiyo sahihi hataingia katika ufalme wa Mungu. Jibu la kichwa cha somo hapo juu ni kwamba Shetani hana nafasi wala mamlaka kuzuia maombi ya watakatifu. Kwa sababu imeandikwa; “BWANA yu mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki.” Mithali 15:29. “Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki
Yakupasa kuwa makini sana usisahau kuishi maisha ya ukamilifu. Unaweza kusahau mambo mengine, lakini jambo hili la ukamilifu yakupasa kuzingatia wakati wote. Tafakari kila wakati je wewe ni mkamilifu?. Ni muhimu kuishi kwa ukamilifu kwa sababu hujui saa wala wakati ambao utaondoka hapa duniani. Siku ile ya mwisho inakuja ghafla na kanisa litanyakuliwa. Hiyo ni siku ambayo hakuna anayeijua. Wale w alio tayari katika ukamilifu hao ndio watakaonyakuliwa. Wale ambao si wakamilifu wataachwa na hatimaye watahukumu na kutupwa katika ziwa la moto. Kuliko utengwe na uso wa Mungu milele ni bora kuishi katika ukamilifu. Kwa sababu hiyo yakupasa kudumu na kuyafanya mambo yote kwa ukamilifu mbele za Mungu na wanadamu. Kwa kufanya hiyo utakuwa umempendeza Mungu na kupata kibali kwake. Ni muhimu kudumu katika ukamilifu wakati wote, ukiwa umelala, unatembea, unakula, unapoongea na watu, unaposafiri, unapokuwa katika shughuli zako mbalimbali. Ndugu, tambua ya kwamba Mungu anakupenda amekupa nafa