Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa; 
"Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka, Mathayo 11:12."  "Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."  Luka 16:16.

Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa Roho Mtakatifu. Lakini hakuweza kuniombea, bali alinijibu akaniambia nimwombe Mungu mwenyewe!. Ijapokuwa nilikuwa ndio nimeokoka na bado ni mtoto mchanga katika wokovu, niliamua kumwomba Mungu kwa imani na bidii. Baada ya siku chache nikiwa katika kuomba nikamkumbusha Mungu anijaze Roho Mtakatifu. Ghafla kwa wakati huo huo nilijazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha mpya. Kwa hiyo kama nisingelikuwa na kiu na kumtafuta Mungu kwa bidii nisingeweza kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo neno alilonena Yesu lilitumia kwangu kama ilivyoandikwa;"Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa". Yohana 7:38-39. Jinsi ya kumtumikia Mungu kwa bidii. Kuna mambo ambayo mkristo anapaswa kuyazingatia katika kumtumikia Mungu. Ni haya yafuatayo; 
1. Kumpenda Mungu. Kwa hiyo mtu atakuwa anampenda Mungu ni lazima aweke nia moyoni mwake kumtafute kwa bidii kila wakati. sababu hiyo imeandikwa; "..., Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza." Mathayo 22:37-38 "Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu." Zaburi 14:2. 

2. Kuutafuta uso wa Mungu kwa maombi na kufunga. "Mtakeni BWANA na nguvu zake,  Utafuteni uso wake sikuzote."  Zaburi 105:4. Mkristo ambaye ameokoka yampasa
 kuweka nia moyoni mwake kwa ajili ya  kumtafuta Mungu kwa bidii. Kwa hiyo ndipo anaweza kuwa na nguvu za Mungu. Ni muhimu kufahamu ya kwamba Mungu huwatia nguvu wale wamtafutao kwa bidii. Kwa mfano tunaweza kujifunza kwa Bwana wetu Yesu Kristo alivyomwomba Mungu wakati wa dhiki. Andiko linasema;  "Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu." Luka 22:43 

3. Kuishi neno la Mungu linavyosema. Kwa sababu hiyo mtu akiishi na kudumu katika neno la Mungu atakuwa ni rafiki wa Yesu. Ndio maana Yesu alipokuwa anafundisha alisema;
"Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuru."   Yohana 15:14. Kwa kuwa BWANA ndiye mwenye haki,  Apenda matendo ya haki,  Wanyofu wa moyo watamwona uso wake." Zaburi 11:7. 

4. Kumwabudu Mungu na kumsifu. Jambo la muhimu mkrsto kulifahamu ni kwamba Mungu husifiwa na viumbe vyote. Kwa kuwa yeye ni Mchungaji na Mtakatifu ameketi juu ya sifa za watakatifu na viumbe vyote. "Na Wewe U Mtakatifu,  Uketiye juu ya sifa za Israel. "

5. Kumtolea Mungu zaka na sadaka. Kuna jambo muhimu la kuzingatia kwa mkristo kabla ya kutoa sadaka. Kwanza sadaka ili ikubaliwe na Mungu ni lazima aishi sawa na maadili ya neno la Mungu. "Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili. Mungu." Luka 11:42 

6. Kutumika katika Karama au kipawa ambacho ulipewa na Mungu.
"Basi kwa kuwa tuna karama mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa ni unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;]ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya; kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha." Warumi 12:6-8. Nitaelezea kuhusu maana ya neno kadiri na neema. Neno kadiri maana yake ni kiasi. Na neno neema ni upendeleo na huru ya Mungu. Kwa hiyo kwa kadiri ya neema ya Mungu anawapa wakristo waliozaliwa mara pili kila mmoja kipawa tofauti na mwingine. "...walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi." 1 Wakorintho 7:7. 

8. Kuishi kwa imani huku ukimtegemea na kumtumaini Mungu. "Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake.Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda."  Yeremia 17:7-8."Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,  Ambao hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu,  Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake,  Tangu sasa na hata milele." Zaburi 125:1-2 

9. Kuwasadia wajane, yatima na masikini. " Dini iliyo safi, isiyo na mbele ya Mungu Baba katika hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa." 
Yakobo 1:27" Hayo yote yampasa mwamini kuyafanya kwa bidii na kumhofu Mungu.

Kwa hiyo sii kwa kujihesabia haki na kujiona kuwa bora kuliko wengine. Mambo yanayofanana na hayo hayapendezi mbele za Mungu, bali ni chukizo kwake. Mkristo akimtumikia Mungu kwa bidii kuna faida nyingi katika maisha yake. 
Hapa nitazieleza baadhi ya faida ambazo mtu anaweza kuzipata; 
1. Ataheshimika mbele ya Mungu.. Ndio maana Yesu alisema;
Mtu akinitumikia, na kuhuisha; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu. Yohana 12:26 

2. Atakuwa ni rafiki wa Mungu. " Maandiko yale yalisemamizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. Yakobo 2:23. Kwa sababu hiyo Ibrahimu aliweza kuwa rafiki wa Mungu kwa sababu alikuwa anampenda na kumtumikia.

3. Atatumiwa na Mungu kutenda mambo makuu ambayo kwa mwanadamu hayawezeka. Ndio maana imeandikwa;
"Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,.."

4. Atakuwa ni mtu anayeishi katika nguvu za Roho Mtakatifu. "Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio." Matendo ya Mitume 5:32. Mitume walikuwa na ushahidi wa kwamba waliopewa Roho Mtakatifu ni wale ambao wamemtii Mungu katika maisha yao. Ina naana ya kwamba wale ambao hawakumtii Mungu hawawezi kumpokea Roho Mtakatifu. 

5. Atakuwa ni mtu mwenye aman na furaha. " Wana amani nyingi waipenda sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza." Zaburi 119:165. “Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa mtu wa ndani,”  Warumi 7:22.
Kwa hiyo mtu anaweza kuwa amani na furaha iwapo anaipenda sheria ya Mungu na kuishi inavyosema. Kwa hiyo tunaweza kuona amani na furaha ya kweli katika Mungu haipatikani katika fedha na mali. 

6. Atakuwa ni mtu mwenye neema ya Mungu. Kwa hiyo Mungu anasema; "Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia." Isaya 65:24 .  Kwa hiyo mtu aliye na neema ya Mungu ni yule anayemtafuta Mungu siku zote na kwa kumpendeza katika maisha yake. sababu hiyo mtu wa nanna hiyo kabla ya kumwomba Mungu hujibiwa; na ikiwa amenena tu atamsikia. Kwa hiyo kuna wakati unasema neno lolote nalo linatokea.

7. Atakuwa ni mtu anayependwa na Mungu. "Nawapenda wale wanipendao,  Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona." Mithali 8:17

8. Atakuwa ni mtu aliyebarikiwa. Mtu ambaye amebarikiwa ni yule ambaye anampenda Mungu na kulitii neno lake.
"kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa." Kumbukumbu la Torati 30:20. 

9. Atakuwa ni mtu mwenye haki. "Nuru imemzukia mwenye haki, Na furaha wanyofu wa moyo." Zaburi 97:11. Aliye na moyo mnyofu ni mtu yule ambaye ni mkamilifu. Kwa kuelezea zaidi ni mtu ambaye hana hila ndani yake. Ndio maana Yesu alipomwona Nathanaeli akimjia alimtambua rohoni ya kuwa ni mtu wa namna gani! Ndio maana imeandikwa; "Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake." Yohana 1:47. 

10. Atakuwa anawezeshwa na Mungu katika mambo yote. Ndio maana Mtume paulo alisema  "Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu"  Wafilipi 4:13. 

11. Atakuwa ni mtu aliye karibu sana na Mungu. "Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili." Yakobo 4:8. Andiko hili linaonesha wazi ya kwamba mtu anayemkaribia Mungu ni yule ambaye ametakaswa. 

12. Bwana atamfunulia mambo yajayo."Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake." Yohana 16:13. 

13. Bwana atamlinda na kumpigania. Ndiyo maana imeandikwa;  "Malaika wa BWANA hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa." Zaburi 34:7."

Maoni

  1. Nimebarikiwa sana Na neno

    JibuFuta
    Majibu
    1. Bila jina23:51

      Nimebarikiwa mtumishi

      Futa
    2. Bila jina12:45

      Nimebarikiwa sana

      Futa
  2. Nimebalikiwa sana

    JibuFuta
  3. Somo zuri sana lina fundisha na kuelekeza namna ya kumtumikia Mungu

    JibuFuta
  4. Bila jina14:37

    Somo Zur sana mtumishi barikiwa na Bwana

    JibuFuta
  5. Bila jina10:43

    Nimebarikiwa sana na ujumbehuu!

    JibuFuta
  6. Bila jina10:39

    Mungu awabariki Sana naawatie nguvu katika kufanya kazi take, SoMo zuri sana

    JibuFuta
  7. Bila jina14:52

    Mungu akufunulie mengi uweze kulisha kondoo zake. Be blessed.

    JibuFuta
  8. Bila jina00:03

    baraka nyingi nimepata katika fundisho hili.barikiwa sana

    JibuFuta
  9. Bila jina19:58

    Barikiwa sana, zaidi ya nilivyobarikiwa Mimi.

    JibuFuta
  10. Bila jina11:04

    Barukiwa Sana ukwel nimejengeka sana

    JibuFuta
  11. Bila jina09:36

    Mungu ni mwema kila wakati namtumainia yeye hataniacha kamwe
    Eeh Mungu🙏 Nakuomba uzidi kunilisha matunda ya Roho mtakatifu Amen..!!

    JibuFuta
  12. Bila jina04:02

    🙏🙏🙏💕

    JibuFuta
  13. Bila jina15:01

    Zaidi sana kumtumikia Mungu Kwa kifupi,,ni kusoma biblia Kwa bidii Kila siku na kutii inachokwambia

    JibuFuta
  14. Bila jina23:14

    Amen,nimebarikiwa sana

    JibuFuta
  15. Bila jina13:37

    Nimebarikiwa sana na neno.

    JibuFuta
  16. Bila jina21:35

    Amen. Ubarikiwe sana

    JibuFuta
  17. Elisha subira12:42

    ubarikiwe mtumishi wa Mungu

    JibuFuta
  18. Elisha subira12:43

    nimebarikiwa

    JibuFuta
  19. Bila jina17:12

    Nimebarikiwa sana mtumishi

    JibuFuta
  20. Bila jina03:10

    Nimebarikiwa sana tena sana na neno .. hallelujah 🙏

    JibuFuta
  21. Bila jina09:54

    Nami nimebarikiwa kwa somo la kumtumikia mungu

    JibuFuta
  22. Bila jina07:29

    Mungu anisaidie nizidi kulijua neno lake ambalo ndo litazidi kuniongoza katika maisha yangu

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...

UPONYAJI WA MAGONJWA.

Chanzo cha magonjwa. Kuna magonjwa yanayotokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya yule mtu ambaye aliyekuwa mngonjwa akamwabia,   “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi”   Yn 5:14.   Ikiwa mtu aliyeokoka akirudia kuishi maisha ya dhambi pepo mchafu anapoona nafasi anachukua pepo wengine na kuingia kwake. Yesu alisema,  “Mara huenda akachukua pamoja naye    pepo    wengine walio waovu    kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”   Mt 12:45.    Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili. Kwa upande mwingine mtu anaweza akawa ni mgonjwa au amekosa lishe.  Uponyaji wa Mungu.                     Mambo ya kuzingatia na kuponywa ni ha...

KUWEKWA HURU KUTOKA DHAMBI YA UZINZI NA UASHARATI.

Jambo la kwanza ninamshukuru Mungu kwa neema yake aliyonipa kufundisha neno lake. Ndungu mpendwa ninajua ya kwamba Mungu alikupenda sana, hata akamtoa Mwana wake wa pekee Yesu Kristo kwa ajili yako ili akukomboe kutoka katika dhambi zote ikiwemo dhambi ya uzinzi na uasherati. Sasa ninakusihi kwa neema ya Mungu fuatana nami kwa makini kuhusu  somo hili nawe utauna utukufu wa Mungu katika maisha yako. Tunaweza kuangalia kwa makini dhambi ya uzinzi na uasharati ambayo mtu akiitenda inaharibu ufahamu wake na hatimaye kuangamia. Mtu anapoteza uhusiano wake na Mungu, mawasiliano kati yake na Mungu yanakatika. Mungu  ni Makatifu hana ushirika na wenye dhambi. “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” Mithali 6:26.   “Lakini maovu yenu yamewafarikisha (yamewatenganisha) ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki  kusikia.”   Isahau 59:2. Atendaye dhambi ya zinaa au  uasherati ...

KUDUMU KATIKA UPENDO WA MUNGU.

Neno la Mungu katika Biblia linatufudisha kuhusu upendo wa Mungu  kwetu. Yeye Mungu ndiye  mwanzo wa upendo kwa sababu alitupenda kwanza. “...alitupenda sisi kwanza”.   1 Yohana 4:19. Jinsi mtu anavyoweza kuwa na upendo wa Mungu. Ni pale mtu anapokuwa amezingatia kudumu katika upendo wa Mungu kama ifuatavyo; 1.Kuishi sawasawa na maagizo yote ya neno la Mungu na kumpenda. “Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;”   Kumbukumbu la Torati 10:12.   “Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwaamuru, kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote”.   Yoshua 22:5. 2. Jambo lingine la kuzingatia ni kwamba yampasa mtu kuyashika maagiz...

MADHARA YA DHAMBI.

Huu ni wakati mwingine ambao Bwana amenijalia kuwepo kwa kusudi lake jema. Nitaelezea katika somo hili kuhusu dhambi ilivyo na madhara kwa mtu aitendaye. Kwanza tuangalie dhambi  ilivyoanza kwa Adamu na Hawa ni wakati walipokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo Mungu aliwakataza wasile. Kwa sababu hiyo dhambi ilisababisha madhara mengi kwa uzao wake na vizazi vyote duniani. Kwa hiyo shida zote zilizopo duniani zimetokana na dhambi. Kutokana na wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa kwa kuwa walitenda dhambi na vizazi vingine vyote vimehesabiwa ni wenye dhambi. Mtu  anazaliwa akiwa na asili ya dhambi kutoka kwa wazazi wa kwanza Adamu na Hawa. Warumi 3:23 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;” Kutokana na sababu hiyo ndio maana kila mwanadamu anakufa sawasawa na Mungu  alivyosema katika kitabu cha Mwanzo 2:16-17 “BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa u...