Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Hakuna laana na mapepo kwa aliyeokoka.

HAKUNA LAANA NA MAPEPO KWA ALIYEOKOKA.

Karibu katika somo hili na kulifuatilia kwa makini nawe utajengwa na kuzidi kuimarika katika neno la Mungu. Nianze kwa kusema kuwa neno la Mungu ni njia, na ni nuru katika maisha yetu. Neno la Mungu limefananishwa na njia kwa sababu mtu akiishi sawasawa na neno  linavyosema anajua anakokwenda na kwamba anafuata njia sahihi na wala hatapotea kamwe. "Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru" (Yn 8:32). Sehemu nyingine neno limefananishwa na nuru. Ikiwa mtu anaishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema, mtu huyo  anatembea katika nuru kungali mchana wala  hatapotea njia. Kwa sababu hiyo neno la Mungu ndilo linatufundisha na kufahamu mambo yote ambayo Mungu alitukirimia katika Kristo Yesu. Mojawapo ya mambo hayo ni; 1. Alituweka huru kutoka laana zote za ukoo, familia na mababu wa zamani. Na si hivyo tu alituweka huru mbali na mikosi na balaa. Ni kwa sababu hiyo Yesu Kristo alifanyika laana itokanayo na torati  kwa ajili yetu. Ndiyo maana andiko linasem...