Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mungu huwatumia na kuwabariki walio waaminifu.

MUNGU HUWATUMIA NA KUWABARIKI WALIO WAAMINIFU.

Fuatana nami katika somo hili ambalo ni la muhimu sana katika maisha yako ya hapa duniani na mbinguni. Mungu anatafuta mtu aliye mwaminifu   ili   amtumie katika kazi yake. Na pia ili mtu aingie mbinguni yampasa kuwa mwaminifu. Ikiwa mtu ni mwaminifu naye huaminiwa na Mungu na wanadamu. Hebu tuangalie ni nani aliye mwaminifu? Jibu la swali hili ni mtu yule awekaye nia moyoni mwake na kuzingatia kuyafanya yote aliyoagiza Mungu katika neno lake. Mtu huyu  anakubalika mbele za Mungu na wanadamu. Anakubalika kwa sababu anampendeza Mungu na wanadamu katika kutenda yaliyo haki. Na ndio maana imeandikwa;   "Mwanamgu, usisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele za wanadamu".   Mithali 3:1,4.   "Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu."  Luka 2:52. Tunaweza kujifunza uaminifu kwa mtumishi wa Mungu Ayubu ambaye aliepuka dhambi na w...