Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ushauri huleta wokovu.

USHAURI HULETA WOKOVU

Karibu katika somo hili ambalo ni muhimu kwa ajili ya kila mtu. Kabla ya kuendelea na somo hili linalohusu ”ushauri huleta wokovu” nitatoa mfano ili uweze kuelewa zaidi. Kila mwanadamu ambaye Mungu alimuumba hawezi kufahamu mambo yote. Pia hawezi kufanya kila jambo. Ndio maana tunaweza kuona katika maisha ya wanadamu anayo elimu ya ujuzi tofauti na mwingine. Kwa sababu hiyo hakuna aliye na ujuzi wa kila kitu. Ndio maana tunaweza kuona kuna mainjinia wa ndege, magari, meli na nyumba. Kuhusu afya ya mtu na matibabu, kuna nadaktari na wauguzi. Kwa hiyo tunaweza kuona makundi hayo yote yanatofautiana katika utendaji wa kazi. Lakini makundi hayo yanajenga na kuboresha maendeleo ya jamii ulimwenguni kote. Kwa upande wa kanisa Mungu amelijali Karama kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo. Kwa sababu hiyo kila mkristo anayo Karama ya  pekee ambayo amepewa kwa ajili ya kanisa. Kwa hiyo unaweza kuona kila mkristo ni muhimu kwa mwingine. Hakuna mtu yeyote anayeweza kujitegemea katika mambo y...