Mkristo wa kweli ni mtu yule ambaye ameokoka na kukionja kipawa cha nguvu za Mungu. Na pia ametoa mwili wake kuwa sadaka kwa Mungu. Kwa sababu hivyo inakuwa ni ibada kwa Mungu. Ndio maana imandikwa kwenye "Warumi 12:1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana." Lakini pia mkristo wa namna hiyo anakuwa na shauku au kiu kwa ajili ya kumwabudu Mungu. Kwa hiyo anapoabudu anahisi uzuri na uwepo wa nguvu za Mungu. Kwa hiyo kutokana matokeo hayo a natamani wakati wote kudumu katika utakatifu. Pia hujilinda na kuepuka kufanya dhambi. Huyapenda mambo ya Mungu kuliko ya dunia. Kwa sababu hiyo anakuwa na bidii kumtafuta Mungu kwa kuomba, kufunga na kumsifu. Jambo lingine hapendezwi na mambo yasiyo ya haki. Wakristo kama hao ndio watakaourithi ufalme wa Mungu. Ni kwa sababu wameshinda majaribu ya yule maovu na ndani yao hamna hila. Hao ndio watu...
Kumjua Mungu kupitia maandiko matakatifu