Yakupasa kuwa makini sana usisahau kuishi maisha ya ukamilifu. Unaweza kusahau mambo mengine, lakini jambo hili la ukamilifu yakupasa kuzingatia wakati wote. Tafakari kila wakati je wewe ni mkamilifu?. Ni muhimu kuishi kwa ukamilifu kwa sababu hujui saa wala wakati ambao Yesu atarudi au wakati utaondoka hapa duniani. Siku ile ya mwisho inakuja ghafla na kanisa litanyakuliwa. Hiyo ni siku ambayo hakuna anayeijua. Wale w alio tayari katika ukamilifu hao ndio watakaonyakuliwa. Na wa ale ambao si wakamilifu wataachwa na hatimaye watahukumu na kutupwa katika ziwa la moto. Kuliko utengwe na uso wa Mungu milele ni bora kuishi katika ukamilifu. kwa sababu hiyo yakupasa kudumu na kuyafanya mambo yote kwa ukamilifu mbele za Mungu na wanadamu. Kwa hiyo kwa kufanywa hivyo unakuwa umempendeza Mungu na kupata kibali kwake. Ni muhimu kudumu katika ukamilifu wakati wote, ukiwa umelala, unatembea, unakula, unapoongea na watu, unaposafiri, unapokuwa katika shughuli zak...
Kumjua Mungu kupitia maandiko matakatifu