Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Tunda la utu wema

TUNDA LA UTU WEMA.

Wema wa Mungu kwa wanadamu. 1.Hili ni tunda ambalo linaonyesha wema wa Mungu kwa waovu na wenye haki, kwa sababu huwatendea    mema. Wakristo ambao wameokoka yawapasa kufanana na yeye kwa kuwatendea watu wote mema.   “Ili mpate kuwa kama wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.”     Mt 5:45. 2.Vile vile ameonyesha wema wake kwa kutuokoa.   “Lakini wema wake Mwokozi wetu    Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa.”   Tit 3:4. 3. Anawavuta kwa wema wake ili wenye dhambi watubu.   “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?”   Rum 2:4. Yatupasayo kuwatendea adui zetu. 1.Kuwasamehe na kuwaombea Baraka.   “Wabarikini wanaowaudi; barikini, wala msilaani.”   Rum 12:14.   “Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi...