Mwaminini Mungu;
Neno hili hapa juu ambalo ni kichwa cha soma hili Yesu ndiye alisema wakati akiwa na wanafunzi wake."Marko 11:21-22 Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka.Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu."
Jinsi ya kuamini.
Kumwamini Mungu ni pale mkristo anapomtumaini na kumtegemea katika moyo wake. Kwa hiyo neno lake Mungu linaonyesha wazi ni mtu mwenye haki ndiye atakayeishi kwa kumwamini yeye. Imeandikwa "Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Waebrania 10:38"
Kutokana na hili somo hapa juu linaonyesha wazi ya kwamba kusudi la Mungu ni mwanadamu aishi kwa kumtumaini na kumtegemea yeye. Ndio maana pia amesema katika "Yeremia 17:5-7 BWANA asema hivi,
Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu. Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake."
Ili mkirsto aweze kumwamimi Mungu kuna mambo muhimu ambayo anapaswa kuyafahamu. Ni haya yafuatayo hapa chini.
1.Kusoma na kufahamu ahadi za Mungu katika neno lake. Ndipo utakuwa unaijenga imani yako na kumwamini Mungu.
2.Kuyajua yale mambo ambayo Mungu aliwaahidi Baba zetu na kuwatendea. Kwa sababu hiyo utafahamu ya kwamba hata sasa atatenda kwako. Kwa hiyo ukiomba kwa imani utapokea.
3.Kuweka kumbukumbu moyoni na kuyaandika yale mambo ambayo Mungu aliwatendea Baba zetu yasemavyo maandiko katika biblia.
Pia waweza kuweka kumbukumbu ya mambo ambayo Mungu ametenda kwa nyakati hizi kwako na hata kwa wengine. Kwa hiyo kwa kufanya hivyo, imani yako haitapungua.
Ukizingatia mambo hayo utakuwa umeijenga imani yako na kumwamini Mungu katika maisha yako.Vilevile tunaweza kujifunza kwa yule akida jinsi alivyoijenga imani yake kupitia mamlaka yake juu ya askari na mtumwa wake. Kwa sababu hiyo alifahamu ya kwamba Yesu anayo mamlaka yale yale na akisema neno mtumishi wake atapona. Na ndivyo ilivyokuwa."Mathayo 8:5-10 Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.
Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.
Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya
Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli."
Mafundisho ni mazuli Sana
JibuFuta