Watoto wa Mungu ambao wamezaliwa mara ya pili watakuwa wanakutana na mitihani ya majaribu. Kwa hiyo mkristo ambaye ataweza kushinda majaribu na kuingia mbinguni ni yule ambaye atazingatia mambo haya yafuatayo; 1. Kuutafuta uso wa Mungu kwa Bidii kila wakati kwa maombi na kufunga. 2. kujifunza neno Mungu kwa bidii na kulifahamu. Mathayo 11:12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. 4. Kudumu kwa kuishi neno la Mungu linavyosema na katika utakatifu." Ufunuo wa Yohana 3:4-5 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake." 5. Kulisimamia neno la Mungu kwa usahihi. Wala usilionee aibu neno la Mungu mbel...
Kumjua Mungu kupitia maandiko matakatifu