Ruka hadi kwenye maudhui makuu

JE SHETANI ANAWEZA KUZUIA MAOMBI?.

Kutokana na somo hili linalohusu je Shetani anaweza kuzuia maombi?  Majibu swali hilo tunawe kuyapata kwa njia ya neno la Mungu ambalo ndio kweli. Ukweli wa neno la Mungu ndio njia sahihi kwa ajili ya kuthibitisha mambo yote. Kwa sababu hiyo yatupasa kuthibitisha mambo yote ambayo tunaamini kama ni sahihi na neno la Mungu. Jinsi ya kufahamu mambo yale tunayoamini kama ni sahihi ni pale yanapokuwa yanaendana au kukubaliana na neno la Mungu. Hiyo ndio imani  sahihi. Lakini ikiwa mambo yoyote tunayoamini yanapingana na neno la Mungu hiyo ni imani isiyo sahihi. Kwa sababu hiyo mtu anakuwa anaishi kinyume na neno la Mungu. Ni muhimu kufahamu ya kwamba mtu ambaye anaishi katika imani isiyo sahihi hataingia katika ufalme wa Mungu.  

Jibu la kichwa cha somo hapo juu ni kwamba Shetani hana nafasi wala mamlaka kuzuia maombi ya watakatifu.
Kwa sababu imeandikwa;
“BWANA yu mbali na wasio haki;
Bali huisikia sala ya mwenye haki.” Mithali 15:29. “Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.” 1 Petro 3:12.  “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.” 1 Petro 3:7.  Kutokana maandiko haya yanaonyesha wazi ya kwamba maombi huzuiliwa kutokana na dhambi. Kwa maneno mengine ina maana ikiwa mtu anaishi maisha ya dhambi, hicho ndio kizuizi cha maombi yake. Jambo lingine ambalo ni kizuizi cha maombi ni pale mtu anapokuwa hamsheshimu mkewe au mumewe. Na si hivyo tu; ikiwa mtu haheshimu watu wengine hicho pia ni kizuizi cha maombi. Pia kuna kizuizi kingine ambacho ni pale mtu anapoomba kwa  nia mbaya au kinyume na neno la Mungu "Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu." Yakobo 4:3.

Kwa sababu hiyo sii sahihi kuamini Shetani anawez a kuzuia maombi ya watakatifu. Ijapokuwa Shatani alimzuia Malaika aliyetumwa kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kumpelekea Danieli majibu ya maombi yake. “Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.”  Danieli 10:12-13. Ni muhimu kufahamu ya kwamba maandiko ya hapa juu  yanaonyesha wazi Mungu huwasikiliza na kuwaangalia wenye haki wanapomwomba yeye. Kwa sababu hiyo maombi ya watakatifu yanafika kwa Mungu bila kuzuiwa na Shetani. 

Maoni

  1. Bila jina06:06

    Ubarikiwe Sana kw somo zuri

    JibuFuta
  2. Bila jina17:51

    Maneno matamu sana

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...