Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KULEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA 1.


Mzazi au mlezi yampasa kufahamu ya kwamba yeye mfano wa kuigwa katika familia. Kwa kawaida watoto hujifunza mambo wanayoyaona au kusikia kwa wazazi, walezi, Waalimu na watu wengine. Kwa hiyo watoto kuwa na maadili mema au mabaya ni kutokana na malezi ya pande zote. Kwa kawaida watoto walivyo bado hawajaweza kupambanua yaliyo mema na mabaya. Lakini wakielimishwa wanaweza kutambua  yaliyo mema na mabaya.

Kuna mambo ya muhimu ambayo mtoto anapaswa kufundishwa ni haya yafuatayo:
1.Kumfundisha mtoto kusema neno asante. Neno asante ni muhimu kwa kila mtu apewapo kitu au kutendewa jambo lolote jema. Kwa hiyo yampasa kusema neno  asante. Kwa kufanya hivyo ni jambo jema na pia ni maadili kwa watu wa rika zote.

Kama mtu mzima hatoi shukrani kwa yale mema ambayo ametendewa huenda yamkini hakulelewa tangu akiwa mtoto ya kwamba yampasa akipewa chakula au amemnunulia nguo aseme asante, au anapopewa kitu chochote na wazazi wake. Usipomlea mtoto katika maadali mema atakapokuwa mtu mzima hataona umuhimu wa kushukuru. Ndio maana kuna baadhi ya watu hawawezi kusema neno la shukrani. Ndio maana kuna mithali inasema umleavyo mtoto ndivyo akuavyo. Kutokana na msemo huo unadhihirisha wazi mambo mawili.


Jambo la kwanza na msingi ni mzazi au mlezi kumlea mtoto katika maadili mema. Kwa sababu hiyo atakua katika maadili. Kwa hiyo katika maisha yake atakuwa anaishi katika maadili mema, ndio maana neno linasema  “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” Mithali 22:6 Lakini ikiwa hatalelewa katika maadili yanayofaa atakuwa hana maadili mema katika maisha yake. Kwa hiyo ni muhimu kwa wazazi au walezi kuwa makini na kuwasaida ili baadae nao waweze kuwa wazazi wenye maadili mema.


2. Kumfundisha mtoto maneno ya Mungu na jinsi ya kumwabudu kwa kufanya maombi, kutoa Sadaka kumsifu na kumshukuru.


3. Kumfundisha kuwa mkarimu. Ni  wakati umempa biskuti au karanga na kumwambia amgawie mtu mwingine. Ikiwa hatafanya hivyo endelea kumzoesha kwa kuchukua ulichompa kama ni karanga na kumgawia mtu mwingine  halafu mbakizie zake . Kwa kufanya hivyo unakuwa umemfundisha kuwa mkarimu. Kwa sababu hiyo siku nyingine akipewa karanga anaweza kumngawia  mtoto mwenzake au mtu mwingine. Hiyo ndiyo njia sahihi ya kuondoa ubinafsi na uchoyo ndani ya nafsi ya mtoto.


Jambo lingine mzazi au mlezi  

anapokuwa anapika ni muhimu kuwa makini asimpe mtoto chakula kabla ya kuwekwa mezani. Nasema hivyo kwa sababu mtoto anapoona chakula anachokipenda sana anaweza kulia na kuomba apewe. Kama utakuwa unampa kidogo huko jikoni kabla ya chakula kuwekwa mezani utakuwa unamjenga mtoto kuwa na tabia ya ubinafsi na uchoyo. Kwa hiyo yakupasa kumwambia asubiri mpaka chakula kiwekwa  mezani naye atapewa. 

Ikiwa mtoto anadokoa chakula jikoni au kitu kingine chochotea si vema kusema huyu
ni mtoto anapokua ataacha. Akiachwa bila kuonywa tabia ya udokozi itakuwa ndani yake hata atapokuwa mtu mzima. Kwa hiyo ni muhimu kumwonya mapema angali mtoto. Kwa kuwa umleavyo mtoto ndivyo akuavyo.

Kuna baadhi ya wapishi wenye uchu wa nyama au chakula wanachokipenda wakati wanapopika  wanakula kwa kiasi fulani huko jikoni. Mtu wa namna hiyo ni mlafi hawezi kurithi ufalme wa Mungu. “...ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” Wagalatia 5:21.

4. Kumfundisha mtoto kula kwa kiasi. Ikiwa kuna chakula anachokipenda sana mpe kwa kiasi cha kushiba. Baada ya kula akiomba kuongezewa chakula mwongezee kidogo sana, au mwambie ulichokula kinatosha. Watoto wadogo huwa wanaelewa wakielekezwa. 

5. Kumfundisha mtoto Kuwa na nidhamu. Awe anaamkia watu ambao ni wakubwa kwake kwa umri. Awaheshemu wageni wanaokuja nyumba kwako bila  kuwasumbua. 

Kwa hiyo ili tuweze kuwa na taifa lenye maadili mema ni lazima mtoto  ajengwa katika maadili mema kuanzia nyumbani. Kwa hiyo siyo sahihi kuwaacha watoto kuangalia picha  katika televisheni na intaneti ambazo siyo salama kwa watoto, zinaharibu maadili ya watoto. Pia kuna baadhi ya machapisho ambayo yana picha na maneno yasiyo salama kwa watoto. Kwa hiyo yakupasa kumlinda na kumwelimisha mtoto wako kwa kumweleza ni yapi yanafaa na yasiyofaa.

Jambo lingine la muhimu yakupasa kutambua kuhusu mtoto wako rafiki zake ni nani! Ili kuchunguza na kubaini tabia za hao rafiki zake. Je? Ni nzuri au ni mbaya. Njia ya kutumia ni kupitia mtoto mwenyewe kwa kuwa na ukaribu naye kwa maongezi. Kwa mfano unaweza ukamuuliza rafiki zake ni nani! hata kama unawafahamu. Kwa hiyo anaweza kukuambia habari za watoto wengine na hata za rafiki zake. Kwa sababu hiyo unaweza kufahamu maadili ya marafiki zake na watoto wengine. Kama atakuwa amekueleza tabia za watoto ambazo ni kinyume na maadili mema mshauri kwa kumwambia hayo wanayoyafanya siyo maadili mema. Pia mkataze asije akayaiga hayo. Vilevile  mwepumshe mtoto wako na marafiki wabaya. Kwa kufanya hivyo utakuwa umemjenga  katika maadili mema.

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...

UPONYAJI WA MAGONJWA.

Chanzo cha magonjwa. Kuna magonjwa yanayotokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya yule mtu ambaye aliyekuwa mngonjwa akamwabia,   “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi”   Yn 5:14.   Ikiwa mtu aliyeokoka akirudia kuishi maisha ya dhambi pepo mchafu anapoona nafasi anachukua pepo wengine na kuingia kwake. Yesu alisema,  “Mara huenda akachukua pamoja naye    pepo    wengine walio waovu    kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”   Mt 12:45.    Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili. Kwa upande mwingine mtu anaweza akawa ni mgonjwa au amekosa lishe.  Uponyaji wa Mungu.                     Mambo ya kuzingatia na kuponywa ni ha...

KUWEKWA HURU KUTOKA DHAMBI YA UZINZI NA UASHARATI.

Jambo la kwanza ninamshukuru Mungu kwa neema yake aliyonipa kufundisha neno lake. Ndungu mpendwa ninajua ya kwamba Mungu alikupenda sana, hata akamtoa Mwana wake wa pekee Yesu Kristo kwa ajili yako ili akukomboe kutoka katika dhambi zote ikiwemo dhambi ya uzinzi na uasherati. Sasa ninakusihi kwa neema ya Mungu fuatana nami kwa makini kuhusu  somo hili nawe utauna utukufu wa Mungu katika maisha yako. Tunaweza kuangalia kwa makini dhambi ya uzinzi na uasharati ambayo mtu akiitenda inaharibu ufahamu wake na hatimaye kuangamia. Mtu anapoteza uhusiano wake na Mungu, mawasiliano kati yake na Mungu yanakatika. Mungu  ni Makatifu hana ushirika na wenye dhambi. “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” Mithali 6:26.   “Lakini maovu yenu yamewafarikisha (yamewatenganisha) ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki  kusikia.”   Isahau 59:2. Atendaye dhambi ya zinaa au  uasherati ...

KUDUMU KATIKA UPENDO WA MUNGU.

Neno la Mungu katika Biblia linatufudisha kuhusu upendo wa Mungu  kwetu. Yeye Mungu ndiye  mwanzo wa upendo kwa sababu alitupenda kwanza. “...alitupenda sisi kwanza”.   1 Yohana 4:19. Jinsi mtu anavyoweza kuwa na upendo wa Mungu. Ni pale mtu anapokuwa amezingatia kudumu katika upendo wa Mungu kama ifuatavyo; 1.Kuishi sawasawa na maagizo yote ya neno la Mungu na kumpenda. “Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;”   Kumbukumbu la Torati 10:12.   “Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwaamuru, kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote”.   Yoshua 22:5. 2. Jambo lingine la kuzingatia ni kwamba yampasa mtu kuyashika maagiz...

MADHARA YA DHAMBI.

Huu ni wakati mwingine ambao Bwana amenijalia kuwepo kwa kusudi lake jema. Nitaelezea katika somo hili kuhusu dhambi ilivyo na madhara kwa mtu aitendaye. Kwanza tuangalie dhambi  ilivyoanza kwa Adamu na Hawa ni wakati walipokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo Mungu aliwakataza wasile. Kwa sababu hiyo dhambi ilisababisha madhara mengi kwa uzao wake na vizazi vyote duniani. Kwa hiyo shida zote zilizopo duniani zimetokana na dhambi. Kutokana na wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa kwa kuwa walitenda dhambi na vizazi vingine vyote vimehesabiwa ni wenye dhambi. Mtu  anazaliwa akiwa na asili ya dhambi kutoka kwa wazazi wa kwanza Adamu na Hawa. Warumi 3:23 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;” Kutokana na sababu hiyo ndio maana kila mwanadamu anakufa sawasawa na Mungu  alivyosema katika kitabu cha Mwanzo 2:16-17 “BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa u...