Maana ya vipimo vya haki ni vipimo vyenye uwiano ulio sawa. Kwa mfano mizani ni kipimo chenye uwiano ulio sawa. Vipimo ambavyo siyo rasmi ambavyo jamii inavitumia kupimia bidhaa kama ndoo, magunia, na kadhalika. Vipimo hivyo ikiwa mtu anavitumia kwa namna isiyo sawa humpunja mkulima wa mazao. Baadhi ya wanunuzi wanapokwenda kununua mazao kama viazi au vituguu wanataka gunia lijazwe kupita ujazo unaotakiwa. Kwa hivyo hushonea ziada wanayoiita LUMBESA. Kutokana na neno la Mungu hapa juu linaonyesha wazi ya kwamba mtu akitenda haki na kuishi sawasawa na sheria na amri za Mungu ataongezewa miaka nyingi ya kuishi hapa duniani. Ina maana ya kwamba hatakufa mapema kwa sababu amemtii Mungu kwa kutenda Sheria na amri zake. Pia atamjalia kuishi kwa amani. Kama nilivyoeleza hapo juu mlanguzi ni mtu anayenunua bidhaa kutoka kwa wakulima kwa bei rahisi na kuwauzia wengine kwa bei ghali ili kupata faida kubwa. Pia inawezekana ikawa ni bidhaa nyingine yoyote hununua na kulangua. Kwa mfanya biasha...
Kumjua Mungu kupitia maandiko matakatifu