Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kuishi maisha ya ukamilifu

KUISHI MAISHA YA UKAMILIFU 1

Yesu alifundisha ya kwamba yatupasa tuwe wakamilifu kama Baba yetu wa Mbinguni alivyo mkamilifu. Huku akiwa ameonyesha wazi upendo wa Mungu kwa wanadamu, jinsi anavyowatendea wema wenye haki na wasio haki. Kwa sababu hiyo yatupasa kutenda kama Mungu kwa kuonyesha upendo wetu kwa watu wote.   Je? Tunawezaje kuonyesha upendo wa Mungu kwa jinsi gani? Jibu la swali hili ni kama ifuatavyo: 1. Kuwapenda watu wote. 2. Kuwatendea mema watu wote. 3, kuwaombea baraka watu wote.  Kamwe! Hatuwezi kumpendeza Mungu kama tunawatakia adui zetu wapatwe na mabaya. Pia hatupaswi kuwaombea maadui zetu ili wapatwe na mabaya. Hayo siyo mapenzi ya Mungu kwetu. Mapenzi ya Mungu katika maandiko yanasema, " Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Maana mkiwap...