Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUJIANDAA KWA AJILI YA IBADA.

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya ibada kwa muda ambao umepangwa. Ili usichelewe Fanya mambo haya;
1 Ikiwa katika familia yako mnao utaratibu mliojiwekea wa kufanya ibada kila siku, kwa mfano saa mbili kamili ya usiku. Ina maana ya kwamba kila mtu anapaswa awe amemaliza shughuli zake kama kupika, kuoga, na kama mmojawapo alikuwa ametoka ni muhimu ahakikishe anarudi nyumbani mapema kabla ya muda wa ibada. Jambo kila mmoja katika familia yampasa injini muda wa ibada na kuzingatia. Kwa hiyo ni muhimu kumheshimu Mungu kwa kuzingatia muda, kama tunavyozingatia muda kwa mambo mengine. 

Kwa mfano mtu amekata mapema kwa ajili ya kusafirishia siku anakuwa ameamka asubuhi na kuwahi basi kabla halijaondoka na kuachwa. Lakini mtu kwa ajili ya ibada anachelewa. Kwa hiyo mtu anakuwa amekosa wa kutumia vizuri muda wa ibada kwa ajili ya Mungu wake. Haipendezi mtu kuwa mwaminifu kwa kutumia muda vizuri kwa mambo mengine mbalimbali, lakini kwa mambo ya Mungu hazingatii muda. Kwa Kufanya hivyo ni kukosa na heshima kwa Mungu. 2. Maandalizi ya ibada kanisani. Fanya haya kabla ya kulala. 
A. Andaa nguo zako. B. Osha au kupiga rangi viatu vyako. C. Andaa sadaka au zaka. D. Andaa biblia yako na mfuko wako.

E. Lala mapema huku ukiwa umeweka nia moyoni mwako muda wa kuamka na itakuwa hivyo. Kwa mfano ukiweka nia ya kwamba utaamka saa kumi na nusu alfajiri. Muda ukifika umeamka. 

F. Mwombe Mungu kwa ajili ya ibada ili akutane na watu wake na kuwasadia. Pia ibada itawaliwe na uwepo wa Mungu. Vilevile omba kwa ajili ya wale watakaokuwa na zamu ya kuongoza ibada ya siku hiyo. Wahi kwenda kanisan dakika 10-15, Kabla ya Muda wa ibada haujafika.

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...