Yakupasa kuwa makini sana usisahau kuishi maisha ya ukamilifu. Unaweza kusahau mambo mengine, lakini jambo hili la ukamilifu yakupasa kuzingatia wakati wote. Tafakari kila wakati je wewe ni mkamilifu?. Ni muhimu kuishi kwa ukamilifu kwa sababu hujui saa wala wakati ambao utaondoka hapa duniani. Siku ile ya mwisho inakuja ghafla na kanisa litanyakuliwa. Hiyo ni siku ambayo hakuna anayeijua. Wale w alio tayari katika ukamilifu hao ndio watakaonyakuliwa. Wale ambao si wakamilifu wataachwa na hatimaye watahukumu na kutupwa katika ziwa la moto. Kuliko utengwe na uso wa Mungu milele ni bora kuishi katika ukamilifu.
kwa sababu
hiyo yakupasa kudumu na kuyafanya mambo yote kwa ukamilifu mbele za Mungu na wanadamu. Kwa hiyo ufanywe umempendeza Mungu na kupata kibali kwake.
Ni muhimu kudumu katika ukamilifu wakati wote, ukiwa umelala, unatembea, unakula, unapoongea na watu, unaposafiri, unapokuwa katika shughuli zako mbalimbali. Ndugu, tambua ya kwamba Mungu anakupenda amekupa nafasi moja tu.
Ni muhimu kufahamu kwamba hiyo ni nafasi ya pekee ambayo ni kwa neema yake Mungu Baba yetu ametupa. Lakini m alaika zake ambao walimwasi Mungu hawajapewa nafasi kama sisi wanadamu. Ndio maana nimesema ni kwa neema ya Mungu ametupa nafasi. Kuishi bila kuwa mkamilifu ni hasara kubwa kuliko hasara zote ambazo mwanandamu anaweza kuzipata hapa duniani. Ndio maana Yesu alisema " .. itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?" Marko 8:36.
Ninakushauri tumia muda wako wote huku ukiwa unadumu katika ukamilifu.
Ninakushauri tumia muda wako wote huku ukiwa unadumu katika ukamilifu.
Jilinde na kuutunza utakatifu wako katika Mungu. Kumbuka nafasi uliopewa ni moja tu ukiipoteza hakuna nyingine, kwa hiyo ni muhimu kuutumia muda vizuri ambao Mungu amekupa kuishi hapa duniani.
Ndugu! usomaye maneno haya nakutakia baraka za Bwana ziwe pamoja nawe. Amina.
Endelea kusoma masomo, bofya hapa;
Asante sana maneno ni ya faraja sana
JibuFuta