Karibu na endelea kujifunza neno la Mungu katika somo hili linalohusu rafiki wa kweli wa Mungu. Yampasa kila mkristo aliyeokoka kufahamu ya kwamba yeye ni rafiki wa Mungu ikiwa anazingatia maagizo ya neno la Mungu kama ifuatavyo; 1. Kumpenda Mungu na kudumu katika kuzishika amri zake. “ Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nimtapenda na kujidhihirisha kwake”. (Yohana 14:21). “...Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuwa kwake, na kufanya makao kwake. Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; …” (Yohana 14:23,24). Kutokana na maandiko ya neno la Mungu kama yanavyosema hapa juu, ni lazima mtu awe na upendo wa kweli kwa Mungu kwa kuzishika amri zake. Ikiwa mtu hatazishika amri za Mungu huyo atakuwa hampendi Mungu na wala si rafiki wa kweli wa Mungu. Kwa sababu hiyo mtu huyo hana upendo wa Mungu ukikaa ndani yake....
Kumjua Mungu kupitia maandiko matakatifu