Hapa tutaangalia mtu ambaye anaweza kuwa na uwezo wa kuomba na kuabudu katika Roho Mtakatifu ni Mkristo ambaye ameokoka na kumtii Mungu kwa kuishi sawasawa na neno lake. Na ndipo anajazwa Roho Mtakatifu, naye Roho atajidhihirisha kwake kama ifuayavyo; 1. Atasikia au kuhisi nguvu ndani yake anapokuja Roho Mtakatifu juu yake. Tunaweza kuona kwa uthibitisho wa maandiko haya yafuatayo, "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu..." Matendo 1:8. Katika andiko tunaweza kuona mtumishi wa Mungu Daudi alipotiwa mafuta na nabii Samweli kuwa Mfalme wa Israel. Roho Mtakatifu alikuja juu yake kwa nguvu. "Ndipo Samweli akaitoa pembe yake ya mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya Bwana ikamjia Daudi kwa nguvu tangu siku ile." 1Samweli16:13. 2. Ataongozwa na Roho Mtakatifu kunena kwa lugha mpya ambayo hajawahi kuisikia wala kufundishwa. "Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia ku...
Kumjua Mungu kupitia maandiko matakatifu