Kwa kusoma mafundisho ya somo hili utajengwa na kuimarishwa katika imani ya neno la Mungu. Kuna jambo la msingi ambalo ni la muhimu kwa kila mkristo aliyeokolewe. Yampasa kwa kila jambo analolifanya alifanye sawasawa na neno la Mungu linavyosema. Mojawapo ya mambo hayo ni ibada katika kuomba, kuabudu, kusifu na kucheza mbele za Mungu. Matumizi yasiyo sahihi ya jina la Yesu. Yatupasa kulitumia jina la Yesu kulingana na kanuni za neno laungu. Hatuwezi kumtukuza na kumeshimu kama tunalitumia jina lake isivyo sahihi. Namna isiyo sahihi ni hili ifuatayo; Ikiwa mtu anatamka na kusema kwa Jina la Yesu ninavunja, ninaharibu na kukemea roho ya dhambi, laana, umaskini, magonjwa na mapepo. Hii siyo njia sahihi inayofaa kuondoa. Njia iliyo sahihi na inayofaa ni kama ifuatavyo: 1. Kuondoa dhambi ni kwa njia ya kuweka nia na kuamua kuziacha na kutubu. "...Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema". (Mithali 28:13). Ijapokuwa Mungu anamsamehe mtu d...
Kumjua Mungu kupitia maandiko matakatifu