Tutajifunza mambo ambayo ni sababu kwa mkristo aliyeokoka kupoteza imani yake. Hapa nitaeleza machache. Anapokuwa na shaka moyoni anapoteza ujasiri wake kwa Mungu. Tunaweza kuona na kujifunza katika andiko hili ambalo linasema, ” Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote. Yakobo 1:6-8.” Hapa ni muhimu tujifunze kisa cha mtume Petro ili kujengwa. Kwa imani alitembea juu ya maji. Lakini ni kwa nini baadae alizama? Jibu la swali hili ni pale alipoona upepo na kuanza kuona shaka moyoni. Kwa sababu aliona shaka asingeweza kuwa na imani. Kwa hiyo mwenye shaka amepoteza imani yake. Mathayo 14:28-31 28 Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. 29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili k...
Kumjua Mungu kupitia maandiko matakatifu