Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kuwa na umoja na mungu

KUWA NA UMOJA NA MUNGU.

Karibu katika somo mbalo linakuhusu wewe kuwa na umoja na Mungu na Yesu Kristo. Umoja ninaofundisha katika somo hili ni ule unaotokana na mtu aliyemwamini Yesu na kuokolewa, na kuamua kuishi sawasawa na maneno ya Mungu  yasemavyo. Mtu kama huyo anakuwa ni mtakatifu kama Mungu alivyo mtakatifu. Ndio  maana Yesu akasema. "Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake." (Yoh 14:23). "Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli  kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake." (1Yoh 2:5) Wale walio watakatifu ndio ambao Mungu amewapa haki ya kuwa na umoja na yeye. Ndio maana imeandikwa, "Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu..." (Yoh 15:3-4). Tunaweza kuona Bwana wetu Yesu Kristo alivyomwomba  Mungu kwa ajili yao watakaomwamini ili wawe na umoja na yeye na Baba. "Wala si hao tu ninaowaombea...