Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

JE SHETANI ANAWEZA KUZUIA MAOMBI?.

Kutokana na somo hili linalohusu je Shetani anaweza kuzuia maombi?  Majibu swali hilo tunawe kuyapata kwa njia ya neno la Mungu ambalo ndio kweli. Ukweli wa neno la Mungu ndio njia sahihi kwa ajili ya kuthibitisha mambo yote. Kwa sababu hiyo yatupasa kuthibitisha mambo yote ambayo tunaamini kama ni sahihi na neno la Mungu. Jinsi ya kufahamu mambo yale tunayoamini kama ni sahihi ni pale yanapokuwa yanaendana au kukubaliana na neno la Mungu. Hiyo ndio imani  sahihi. Lakini ikiwa mambo yoyote tunayoamini yanapingana na neno la Mungu hiyo ni imani isiyo sahihi. Kwa sababu hiyo mtu anakuwa anaishi kinyume na neno la Mungu. Ni muhimu kufahamu ya kwamba mtu ambaye anaishi katika imani isiyo sahihi hataingia katika ufalme wa Mungu.   Jibu la kichwa cha somo hapo juu ni kwamba Shetani hana nafasi wala mamlaka kuzuia maombi ya watakatifu. Kwa sababu imeandikwa; “BWANA yu mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki.” Mithali 15:29. “Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki
Machapisho ya hivi karibuni

USISAHAU KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Yakupasa kuwa makini sana usisahau kuishi maisha ya ukamilifu. Unaweza kusahau mambo mengine, lakini jambo hili la ukamilifu yakupasa kuzingatia wakati wote. Tafakari kila wakati je wewe ni mkamilifu?. Ni muhimu kuishi kwa ukamilifu kwa sababu hujui saa wala wakati ambao utaondoka hapa duniani. Siku ile ya mwisho inakuja ghafla na kanisa litanyakuliwa. Hiyo ni siku ambayo hakuna anayeijua. Wale w alio tayari katika ukamilifu hao ndio watakaonyakuliwa. Wale ambao si wakamilifu wataachwa na hatimaye watahukumu na kutupwa katika ziwa la moto.  Kuliko utengwe na uso wa Mungu milele ni bora kuishi katika ukamilifu.   Kwa sababu  hiyo yakupasa kudumu na kuyafanya mambo yote kwa ukamilifu mbele za Mungu na wanadamu.  Kwa kufanya hiyo utakuwa umempendeza  Mungu na kupata kibali kwake.  Ni muhimu kudumu katika ukamilifu wakati wote, ukiwa umelala, unatembea, unakula, unapoongea na watu, unaposafiri, unapokuwa katika shughuli zako mbalimbali. Ndugu, tambua ya kwamba Mungu anakupenda amekupa nafa

HATUA ZA KUUKULIA WOKOVU NA NEEMA YA MUNGU

Mwaminini Mungu; Neno hili hapa juu  ambalo ni kichwa cha soma hili Yesu ndiye alisema wakati akiwa na wanafunzi wake. " Marko 11:21-22 Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka. Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu." Jinsi ya kuamini. Kumwamini Mungu ni pale mkristo anapomtumaini na kumtegemea  katika mawake   yake. Kwa hiyo neno lake Mungu linaonyesha wazi ni mtu mwenye haki ndiye atakayeishi kwa kumwamini yeye . Imeandikwa "Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Waebrania 10:38" Kutokana na hili andiko hapa juu linaonyesha wazi ya kwamba kusudi la Mungu ni mwanadamu aishi kwa kumtumaini na kumtegemea yeye. Ndio maana pia amesema katika  " Yeremia 17:5-7 B WANA asema hivi,  Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu. Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake  Na moyoni mwake amemwacha BWANA. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali at

KJIANDAA KWA AJILI YA IBADA.

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya ibada kwa muda ambao umepangwa. Ili usichelewe Fanya mambo haya; 1 Ikiwa katika familia yako mnao utaratibu mliojiwekea wa kufanya ibada kila siku, kwa mfano saa mbili kamili ya usiku. Ina maana ya kwamba kila mtu anapaswa awe amemaliza shughuli zake kama kupika, kuoga, na kama mmojawapo alikuwa ametoka ni muhimu ahakikishe anarudi nyumbani mapema kabla ya muda wa ibada. Jambo kila mmoja katika familia yampasa injini muda wa ibada na kuzingatia. Kwa hiyo ni muhimu kumheshimu Mungu kwa kuzingatia muda, kama tunavyozingatia muda kwa mambo mengine.  Kwa mfano mtu amekata mapema kwa ajili ya kusafirishia siku anakuwa ameamka asubuhi na kuwahi basi kabla halijaondoka na kuachwa. Lakini mtu kwa ajili ya ibada anachelewa. Kwa hiyo mtu anakuwa amekosa wa kutumia vizuri muda wa ibada kwa ajili ya Mungu wake. Haipendezi mtu kuwa mwaminifu kwa kutumia muda vizuri kwa mambo mengine mbalimbali, lakini kwa mambo ya Mungu hazingatii muda. Kwa Kufanya hivyo ni kukosa

MKRISTO WA KWELI.

Mkristo wa kweli ni mtu yule ambaye ameokoka na kukionja kipawa cha nguvu za Mungu. Na pia ametoa mwili wake kuwa sadaka kwa Mungu. Kwa sababu hiyo kwa kufanya hivyo ni ibada kwa Mungu.  Ndio maana imandikwa kwenye  "Warumi 12:1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana."  Lakini pia  anakuwa na shauku au kiu kwa ajili ya kumwabudu Mungu. Kwa sababu hiyo, wakristo wa namna hiyo wanapokuwa katika kumwabudu Mungu watauona uzuri wa Mungu na uwepo wa nguvu zake. Wanatamani wakati wote kudumu katika utakatifu. Pia hujilinda na kuepuka kufanya dhambi. Huyapenda mambo ya Mungu kuliko ya dunia.  Vilevile huwa ni watu mwenye bidii katika kumtafuta Mungu kwa kuomba, kufunga na kumsifu Mungu. Jambo lingine hawapendezwi na mambo yasiyo ya haki. Watu kama hao ndio watakaourithi ufalme wa Mungu. Ni kwa sababu wameshinda majaribu ya yule maovu na ndani yao hamna hila. Hao ndio wa

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa Roh

MUNGU NDIYE ATENDAYE MIUJIZA.

Tunaweza kuona ya kwamba vitu vyote ambavyo Mungu ameviumba ni muujiza kwetu. Pia aliumba kwa namna ya pekee jua, mwezi, nyota na sayari nyingine mbalimbali ambazo  aliziweka juu ya anga, huku zikiwa zinaning’inia bila kushikiliwa na kitu chochote, wala hazidondoki. Pia bahari nayo imekaa mahali ilipoamriwa bila kuvuka mpaka alioiwekea Bwana. Kwa hiyo tunapoona uumbaji wa vitu vyote ambavyo Mungu aliviumba vinashangaza, navyo ni ishara  kwetu ya kutosha na kutambua ya kwamba Mungu yupo. Kwa sababu hiyo yatupasa kufahamu ya kwamba yeye ndiye mwenye uwezo wote, yeye hutenda mambo yote sawasawa na mapenzi yake. Kwa hiyo tunaweza kuona Sababu ya Mungu kufanya muujiza kwa mkono wa Musa mbele ya Farao na Wamisri. Mungu akamwambia Farao; “lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu hii hii, ili nikuonyeshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote.” Kutoka 9:16. Kutokana na andiko hili hapa juu linazungumzia Mungu alifanya miujiza ili kumwonyesha Farao uweza wake. Na Kusud

KULEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA 1.

M zazi au mlezi yampasa kufahamu ya kwamba yeye mfano wa kuigwa katika familia. Kwa kawaida watoto hujifunza mambo wanayoyaona au kusikia kwa wazazi, walezi, Waalimu na watu wengine. Kwa hiyo watoto kuwa na maadili mema au mabaya ni kutokana na malezi ya pande zote. Kwa kawaida watoto walivyo bado hawajaweza kupambanua yaliyo mema na mabaya. Lakini wakielimishwa wanaweza kutambua  yaliyo mema na mabaya. Kuna mambo ya muhimu ambayo mtoto anapaswa kufundishwa ni haya yafuatayo: 1.Kumfundisha mtoto kusema neno asante. Neno asante ni muhimu kwa kila mtu apewapo kitu au kutendewa jambo lolote jema. Kwa hiyo yampasa kusema neno  asante. Kwa kufanya hivyo ni jambo jema na pia ni maadili kwa watu wa rika zote. Kama mtu mzima hatoi shukrani kwa yale mema ambayo ametendewa huenda yamkini hakulelewa tangu akiwa mtoto ya kwamba yampasa akipewa chakula au amemnunulia nguo aseme asante, au anapopewa kitu chochote na wazazi wake. Usipomlea mtoto katika maadali mema atakapokuwa mtu mzima hataona um