Jambo la kwanza ninamshukuru Mungu kwa neema yake aliyonipa kufundisha neno lake. Ndungu mpendwa ninajua ya kwamba Mungu alikupenda sana, hata akamtoa Mwana wake wa pekee Yesu Kristo kwa ajili yako ili akukomboe kutoka katika dhambi zote ikiwemo dhambi ya uzinzi na uasherati. Sasa ninakusihi kwa neema ya Mungu fuatana nami kwa makini kuhusu somo hili nawe utauna utukufu wa Mungu katika maisha yako. Tunaweza kuangalia kwa makini dhambi ya uzinzi na uasharati ambayo mtu akiitenda inaharibu ufahamu wake na hatimaye kuangamia. Mtu anapoteza uhusiano wake na Mungu, mawasiliano kati yake na Mungu yanakatika. Mungu ni Makatifu hana ushirika na wenye dhambi. “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” Mithali 6:26. “Lakini maovu yenu yamewafarikisha (yamewatenganisha) ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” Isahau 59:2. Atendaye dhambi ya zinaa au uasherati ...
Yakupasa kuwa makini sana usisahau kuishi maisha ya ukamilifu. Unaweza kusahau mambo mengine, lakini jambo hili la ukamilifu yakupasa kuzingatia wakati wote. Tafakari kila wakati je wewe ni mkamilifu?. Ni muhimu kuishi kwa ukamilifu kwa sababu hujui saa wala wakati ambao utaondoka hapa duniani. Siku ile ya mwisho inakuja ghafla na kanisa litanyakuliwa. Hiyo ni siku ambayo hakuna anayeijua. Wale w alio tayari katika ukamilifu hao ndio watakaonyakuliwa. Wale ambao si wakamilifu wataachwa na hatimaye watahukumu na kutupwa katika ziwa la moto. Kuliko utengwe na uso wa Mungu milele ni bora kuishi katika ukamilifu. kwa sababu hiyo yakupasa kudumu na kuyafanya mambo yote kwa ukamilifu mbele za Mungu na wanadamu. Kwa hiyo ufanywe umempendeza Mungu na kupata kibali kwake. Ni muhimu kudumu katika ukamilifu wakati wote, ukiwa umelala, unatembea, unakula, unapoongea na watu, unaposafiri, unapokuwa katika shughuli zako mbalimbali. Ndugu, tambua ya kwamba Mungu ana...