Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kukumbukwa na Mungu

KUKUMBUKWA NA MUNGU

Kuna watumishi wa Mungu katika biblia ambao walikumbukwa na Mungu. Ni kwa sababu walikuwa na sifa njema mbele zake. Mojawapo ya sifa hizo walikuwa wameyatoa maisha yao kwake ili kumpendeza. Kwa sababu hiyo Waliisha sawasawa na neno lake.  Walikuwa wakitii kwa kila neno ambalo Mungu aliwaagiza, ndio maana wamekumbukwa kwa  ajili ya mema yao katika vizazi vingi. Kwa sababu hiyo watu kama hao Mungu alipendezwa nao. Wamekuwa kielelezo kwa watu wengine. Watu kama hao wakiondoka hapa duniani watakumbukwa pia na wanadamu. Hapa nitawataja baadhi ya watu katika biblia ambao wamekumbukwa  ni Ibraimu, Musa na Daudi. Ni vema kufahamu ya kwamba mtu mwenye sifa njema amepanda wema katika maisha yake na vizazi vyake.  Kwa soma hili tunajifunza ya kwamba yatupasa tuangalie jinsi tunavyo enenda mbele za Mungu. Ili tukiondoka hapa duniani tuache sifa njema mbele za Mungu na wanadamu. Kwa sababu ya sifa njema uzao wako unabarikiwa. Kuna watu wengine hawakutii maagizo ya Mungu wamekumbu...