Kuhusu somo hili tuweza kuona,nini maana ya madhabahu na ilivyotumika.
Madhabahu ni mahali palipotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kumtolea Mungu sadaka mbali mbali za kuteketezwa kama sadaka za dhambi na amani. Jambo hilo lilifanyika wakati wa agano la kale. Mungu ndiye aliyetoa maelekezo ya kuijenga madhabahu kwa kutumia mawe.
Wakati huo Musa lipewa hayo maelekezo, “Kumbukumbu la Torati 27:5-75 Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake.
6 Jenga hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee Bwana, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;
7 ufanye na sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi mbele za Bwana, Mungu wako."
Kwa hiyo sadaka ziliwekwa juu ya madhabahu na kutekelezwa mbele za Bwana.
Kwa wakati huu wa agano jipya hatujengi tena madhabahu ya mawe na kuteketeza sadaka juu yake.
Ni kwa sababu Yesu Kristo alikuja kama sadaka ya ulimwengu na kufa msalabani. Kwa sababu hiyo kwa damu yake iliyomwagika pale msabani kwa ajili yakutusafisha dhambi zetu. Jambo hili alithibitisha Yohana mbatizaji kama ilivyoandikwa katika kitabu cha "Yohana 1:29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!" Pia imeandikwa katika "1 Yohana 1:7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote."
Neno madhabahu linatumika kwa namna isiyo sahihi katika nyumba ya ibada. Kwenye nyumba ya kuabudia ile sehemu ya mbele kuitwa ni madhabahu siyo sahihi. Wakati huu wa agano jipya hakuna madhabahu na wala hatujengi madhabahu. Kwa sababu hiyo madhabahu ilijengwa na kutumika wakati wa agano la kale. Ndio maana hatutoi sadaka za kutekeleza.
Jambo lingine ni kuhusu damu ya Yesu ambayo ilimwagika mara moja tu pale msalaba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Kwa sababu hiyo ni muhimu kuwa makini na kuzingatia neno la Mungu linavyosema kuhusu matumizi ya damu ya Yesu. Pia ni muhimu kuepuka kuitumia damu ya Yesu au neno madhabahu kwa namna isiyo sahihi bila uthibitisho wa neno la Mungu.
Siyo sahihi kuitumia damu ya Yesu wakati wa kukemea pepo na kusema kwa damu ya Yesu pepo toka au kumwombea mtu damu ya Yesu imfunike na kumlinda. Yesu aliagiza akasema mtatoa pepo kwa jina langu. Wala hakusema mtatoa pepo kwa damu yangu.
Ni muhimu kujifunza neno la Mungu kwa bidii na kulifahamu. Kwa hiyo kupita neno la Mungu ndio uthibitisho katika maisha yako, na kwa kila jambo unalolifanya. Kwa sababu hiyo zingatia kwa kila jambo unalolifanya ni sawa na neno la Mungu.
Ni muhimu kufahamu kazi ya damu ya Yesu ni kuosha dhambi. Ndio maana imeandikwa katika, "Ufunuo wa Yohana 1:5 ... kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,"
Endelea kusoma zaidi,
Kwasasa hivi hakuna madhabahu
JibuFuta