Ruka hadi kwenye maudhui makuu

AHADI ZA MUNGU KWA AJILI YAKO

Tunaposoma katika biblia tunaweza kuona ahadi mbalimbalii ambazo Mungu ameahidi kwa ajili watoto wake. Ni wale ambao wameokolewa na Yesu na kuishi sawasawa na neno la Mungu.Kwa sababu wamedumu katika neno lake anawatimizia ahadi zake.

Lakini ili yatimie yale aliyoahidi katika neno lake kuna mambo ya kuzingatia.Ni haya yafuatayo;
1. Kusoma neno lake na kufahamu ahadi zake.

2. Kuamini yale aliyoahidi katika neno lake.Tunawe kuona jinsi Ibrahimu alivyomwamini Mungu, katika kitabu cha “Warumi 4:20-22.Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; 
huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.”

3. Kuomba kwa imani sawasawa na yale aliyoahidi. Daudi ni kielelezo cha kuigwa aliomba akasema, “Dua yangu na ifike mbele zako,Uniponye sawasawa na ahadi yako.ZABURI 119:170.” Aliomba hivyo kwa sababu alikuwa anajua ahadi za Mungu.

4. Kuomba mapenzi yake yatimie sawasawa na ahadi zake. Lakini mtu anakuwa ameomba vibaya pale anaposema lazima atafanya. Kusema hivyo siyo sahihi kwa sababu yeye hufanya yote kwa mapenzi yake. Ndio maana Yesu alifundisha jinsi ya kuomba akasema,“Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Mathayo 6:9-10.”

5.Kumtegemea na kumtumaini Mungu kwa yale yote aliyoahidi. Daudi alimtumaini Mungu katika neno akasema “Nami nitamjibu neno anilaumuye, Kwa maana nalitumainia neno lako. Zaburi 119:42.” Kwenye kitabu cha Yeremia Mungu amesema,
“Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.Yeremia 17:7.”
Kutokana na andiko hili linamaanisha ya kwamba atakuwa amepokea baraka za Bwana. Ina maana anayapokea yale aliyokuwa anayahitaji kwa kumtegemea na kumtumaini Mungu.

Kumbuka ni muhimu kusoma neno la Mungu na kuzingatia uliyojifunza katika somo hili. Ikiwa utafanya hivyo utafahamu ahadi za Mungu. 

Hapa nitazitaja baadhi ya ahadi
kama ifuatavyo;
1.Ahadi ya uponyaji.
“Mithali 3:7-8
Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana,ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.”
“Kutoka 23:25 Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.”

2.Ahadi ya ulinzi na kuokolewa.
“Zaburi 34:7
Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.” 
“Zaburi 50:15
Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...