Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUBATIZWA NA KUSHIRIKI MEZA YA BWANA

 Je ni nani anaweza kubatizwa na kushiriki meza ya Bwana?

Kabla ya kujibu swali hili tunaweza kuona kwanza kuna makundi mawili ambao ni watu wakubwa na watoto.Hawa wote wanahita wakati sahihi wa kubatizwa na kushiriki meza ya Bwana.

Kanuni ya kuzingatia ya neno la Mungu ni moja kwa watu wakubwa na watoto, ambayo ni kumwamini Yesu na kutubu dhambi zao. Lakini kwa upande wa watoto wadogo bado hawajafikia ukomavu, kujitegemea na kuamini. Kwa hiyo ni jukumu la wazazi, walezi na kanisa kuendelea kuwafundisha neno la Mungu. Na hatimaye wakati utafika na kuweza kupambanua neno na kumtegemea Mungu katika maisha yao.

Kwa sababu hiyo siyo sahihi kuwabatiza na kuwashirikisha meza ya Bwana watoto. Yesu alifundisha katika kitabu cha“Marko 16:16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.”

Kama alivyosema Yesu hapa juu anayeami ndiye atabatizwa. Kwa sababu hiyo watoto bado hajafikia umri ambao wanaweza kuamini na kujitegemea katika neno la Mungu.  

Pia kwa upande wa watu wakubwa baadi yao hawastahilli kushiriki meza ya Bwana kwa sababu ni wenye dhambi. Kwa hiyo ni muhimu kutambua meza ya Bwana ni takatifu. Kwa hiyo katika hao wenye dhambi walioshiriki baadhi yao waliugua na kufa.

Ndiyo maana imeandikwa katika kitabu cha “1 Wakorintho 11:27-31

27 Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.

28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.

29 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili.

30 Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala.

31 Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa.”

Ni muhimu kufahamu maana ya neno "kupambanua" linamaanisha kutofautisha vizuri kati ya mambo mawili au zaidi kwa kutumia akili, maarifa, au uchambuzi wa kina.

Pia ni kuchambua kwa undani ili kuelewa tofauti au maana halisi ya jambo. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...