Kuna watumishi wa Mungu katika biblia ambao walikumbukwa na Mungu. Ni kwa sababu walikuwa na sifa njema mbele zake. Mojawapo ya sifa hizo, walikuwa wameyatoa maisha yao kwake ili kumpendeza. Kwa sababu hiyo Waliisha sawasawa na neno lake.
Walikuwa wakitii kwa kila neno ambalo Mungu aliwaagiza, ndio maana wamekumbukwa kwa ajili ya mema yao katika vizazi vingi. Kwa sababu hiyo watu kama hao Mungu alipendezwa nao.
Wamekuwa kielelezo kwa watu wengine. Watu kama hao wakiondoka hapa duniani watakumbukwa.
Hapa nitawataja baadhi ya watu katika biblia ambao wamekumbukwa ni Ibraimu, Musa na Daudi.
Ni vema kufahamu ya kwamba mtu mwenye sifa njema, amepanda wema katika maisha yake na vizazi vyake.
Kwa soma hili tunajifunza ya kwamba yatupasa tuangalie jinsi tunavyo enenda mbele za Mungu. Ili tukiondoka hapa duniani tuache sifa njema mbele za Mungu na wanadamu. Kwa sababu ya sifa njema uzao wako unabarikiwa.
Kuna watu wengine hawakutii maagizo yake wamekumbukwa kwa ajili ya makosa yao kwa vizazi vingi. Hao waliacha sifa mbaya. Hapa nitamtaja mmoja wapo ambaye ni Mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati. Alitajwa mara nyingi kwa maovu yake aliyoyatenda ambayo yameandikwa katika vitabu vya Wafalme wa kwanza na Wafalme wa pili.
Jambo la kukumbuka.Ili Mungu akukumbuke yakupasa kuwa na sifa njema. Ambayo inatokana na kuyatii maagizo yake.
Shirikisha wengine somo hili.Mungu akubariki.
Amina
JibuFuta