Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UKUU WA YESU

Yesu ni Mungu.

 - Yeye alikuwako.

- Yeye yuko milele.  

Alikuwa tayari yupo.

Yesu alithibitisha ya kwamba yeye ni nani kama alivyosema kwenye
"Ufunuo wa Yohana 22:13  Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho" .

Yeye ni mwanzo wa vitu vyote. Yeye aliumba vitu vyote.

Yohana 1:1-3, 18

1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.


2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.


3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.


Wakolosai 1:16-17

16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.


17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.


Kwa sababu Yesu aliumba vitu vyote vya mbinguni na duniani ni uthibitisho ya kwamba yeye ni Mungu mwana pekee wa kweli.


Yesu ni Mungu Mwana pekee.

Yohana 1:18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.


'YOHANA 14:8 -10

8 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.'  


9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo Aliyeniona mimi amemwona Baba basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba'


10 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.'


Anayo mamlaka yote.

Mathayo 28:18  Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.


Anayo mamlaka ya kuwapa watu wote uzima wa milele kwa kila aaminiye.


1) Yeye anao huo uzima.

Yohana 1:4.

4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.


Yohana 17:2.

2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.'


1 Yohana 5:11-12

11 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.


12 Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.


Anayo mamlaka ya kusamehe mdhambi.

Marko 2:5, 10

5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.


10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),


Anayo mamlaka ya kufufua wafu na kuhukumu.

 

1) Alifufua wafu mmojawapo ni Lazaro.

Yohana 11:21, 23, 25-26

21 Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.


23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka.


25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;


26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?


Yohana 11:38, 41, 43-44

38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.


41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.


43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.


44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.


2) Siku ya mwisho atafufua wafu wote na kuwahukumu watu wote.

Yohana 5:22-29

22 Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana (Yesu) hukumu yote;


23 ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka.


24 Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.


25 Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.


26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.


27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.


28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.


29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.


Anatawala milele.

Luka 1:31-33

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.


32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.


33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.


Danieli 7:14  Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.


Yeye ndiye anayeokoa wanadamu.

'MATENDO 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.'


'MATHAYO 1:21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.'


Kila goti litapigwa na kila ulimi utamkiri.

Wafilipi 2:9-11

9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;


10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;


11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.


Kuingia ufalme wa Mungu ni kupitiaYesu Kristo.

 Yohana 14:6  Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII

Kutokana na kichwa cha somo hapo juu mkristo ataweza kumtumikia Mungu kwa bidii kama ataweka nia katika  moyo wake.   Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa Roho Mtakatifu. Lakini hakuweza kuniombea, bali alipojibu ya kwamba nimwombe ...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...

UPONYAJI WA MAGONJWA.

Chanzo cha magonjwa. Kuna magonjwa yanayotokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya yule mtu ambaye aliyekuwa mngonjwa akamwabia,   “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi”   Yn 5:14.   Ikiwa mtu aliyeokoka akirudia kuishi maisha ya dhambi pepo mchafu anapoona nafasi anachukua pepo wengine na kuingia kwake. Yesu alisema,  “Mara huenda akachukua pamoja naye    pepo    wengine walio waovu    kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”   Mt 12:45.    Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili. Kwa upande mwingine mtu anaweza akawa ni mgonjwa au amekosa lishe.  Uponyaji wa Mungu.                     Mambo ya kuzingatia na kuponywa ni ha...