Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi  kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea  Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi  maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa ajili ya kufanya uamuzi. Ndio maana Yesu  alipokuwa akifundisha  alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi kwa hiari maisha ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi.
"Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya,  kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33.

Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana  Mungu alimwambia Musa, "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"   Walawi 19:2.

Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema; “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao”  Zaburi 16:3.
"Bwana wetu  Yesu Kristo anakazia jambo  hilo  akisema, “ Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama baba yenu wa mbinguni alivyo mtakatifu” Mathayo 5:48

Mambo ya kuzingatia.
1Kujifunza neno. “ Tena mtaifahamu kweli (Neno) nayo hiyo kweli itawaweka huru. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli” Yohana 8:32. Hiyo kweli inakuweka huru mbali na dhambi, hutasikia hukumu ndani yako. “Wapenzi mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu” 1Yohana 3:21.

2. Kuamini neno linavyosema.
“Basi ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake (mbingini), na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha yake, kama vile alivyosema”. Ebrania 4:1-3.

3.
 Kutenda neno kama linavyosema. “Yesu akajibu,  akawaambia, Mtu akinipenda, atalishika      neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. Mtu asiyenipenda, hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalosikia silo langu, ila ni la Baba aliyenipeleka"  Yohana 14:23-24. Hapa chini kuna andiko lifuatalo ambalo si kwamba linamhusu kijana tu, bali linamhusu kila mtu aliyeokoka yampasa kuwa safi na kulitii neno la Mungu. Andiko linasema “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii akilifuata neno lako”. Zaburi 119:9. 

4. Kuliweka neno la Mungu moyoni. Kuliweka neno la Mungu moyoni litakuongoza na wewe utaepuka maovu. “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi”. Zaburi 119:11. Kwa kuwa neno linamwongoza mtu linamsababisha alitii na kuishi maisha safi ndio mana Yesu aliwaambia wanafunzi wake “Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia”. Yohana 15:3.

5. 
Kuomba kila siku. Tunapoomba Mungu anatupa uwezo wa kushinda majaribu yote. Ndio maana imeandikwa,"Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” Wafilipi 4:23. Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni, roho i radhi lakini mwili ni dhaifu”.  Mathayo 26:41. 

Maoni

  1. Ninabarikiwa na Neno hili,nataman kujua principle yakuomba kila sku ndio kukesha???maana imeunganshwa point na andiko hilo

    JibuFuta
  2. Nmebarikiwa sana na neno hili, Mungu na anisaidie niishi maisha ya utakatifu.
    Be blessed

    JibuFuta
  3. Nimejifunza niliyokua siyatambui MUNGU akubariki

    JibuFuta
  4. Nimebarikiwa sana endelea kututumia masomo namnahii Mungu akubariki

    JibuFuta
  5. Ameeen 🙏🙏🙏 mtumishi MUNGU AZIDI KUKUBARIKI

    JibuFuta
  6. Somo Zuri Sana Mtumishi Ubarikiwe

    JibuFuta
  7. Ubarikiwe sana kwa Shule hii
    Nmejifunza

    JibuFuta
  8. AMEN!! MUNGU akubariki kwa baraka zote

    JibuFuta
  9. Bila jina23:16

    Ubarikiwe sana mtumishi
    Usichoke kusema kweli

    JibuFuta
  10. Bila jina14:06

    Nmebarikiwa sana na neno hili mungu akubariki na akuweke uzidi kunifunza zaidi Be blessed

    JibuFuta
  11. Bila jina00:35

    Ameen

    JibuFuta
  12. Novatus12:19

    Ubarikiwe mtu wa Mungu, kwa somo zuri.
    Ni kweli kabisa Yesu atakapokuja mara ya pili, atakuja kuwachukua watakatifu waliozifua nguo zao ktk damu ya mwanakondoo.

    JibuFuta
  13. Bila jina15:24

    Ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu Kwa somo hili kweli nimejua Jinsi ya kuishi MAISHA ya utakatifu Be blessed man of God 🙏🙏🙌🙌

    JibuFuta
  14. Bila jina23:58

    Nimebarikiwa na ujumbe be blessed

    JibuFuta
  15. Bila jina14:31

    Hakika tutaishi katika IMANI ya kweli kama baba asemavyo be blessed

    JibuFuta
  16. Bila jina17:11

    Mungu akubariki Sana nimejifunza jinsi yakuishi maisha ya utakatifu

    JibuFuta
  17. Bila jina20:30

    Hakika nimasomo yenye faraja kubwa mno bwana awabariki sana

    JibuFuta
  18. Bila jina18:01

    Mungu akubariki sana mtumishi wa Mungu hakika nimepata kitu kupitia hili soma

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa Roh

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawasawa na maagizo, sheria na taratibu . I