- Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu. “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu. Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.” Kum 7:9, 12. “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. Isa 55:11"
- Tabia ya mtu mwaminifu.
- 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawasawa na maagizo, sheria na taratibu . Ikiwa ni mtu aliyeajiriwa katika kazi za nyumbani au ya serikali anafanya kazi ipasavyo, si mwizi, mpokea rushwa, mdhulumaji na wala si mwenye hila. Unaweza kuona ilivyoandikwa kuhusu mtumishi aliyeajiriwa kazi za nyumbani ambaye alipaswa kufanya kwa uaminifu. “Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.” Mt 24:45-46.
- 2. Hatendi dhambi.Yusufu mtumishi wa Potifa kwa kuwa alikuwa mwaminifu aliposhawishiwa na mke wa Potifa ili kufanya naye dhambi ya uzinzi alikataa. “....mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, lala nami. Lakini alikataa akamwambia....Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?” Mwa 39:7-9.
- 3. Hachukui kitu cha mtu mwingine, iwe ni fedha, mali, au kitu kingine chochote ambacho si halali yake. Akitoa fedha kwa ajili ya malipo yoyote na akarudishiwa pesa ya ziada hurudisha kiasi kilichozidi. Ikiwa amemwona mtu ambaye amedondosha fedha au amepoteza kitu chochote humrudishia. Kwa kufanya hivyo analitii na kulitenda neno la Mung linavyosema, “Umwonapo ng’ombe wa nduguyo au kondoo wake akipotea....sharti umrudishe kwa nduguyo. Na kwamba yule nduguyo hayuko karibu nawe, na ukiwa humjui, umchukue kwenu nyumbani kwako, uwe naye hata aje nduguyo kumtafuta, nawe mrudishie....tena fanya vivyo kwa kila kitu kilichopotea cha nduguyo,....” Kum 22:1-3.
- Umuhimu wa kuwa mwaminifu.
- Mkristo ambaye ameokoka akiwa ni mwaminifu, Mungu anamwamini na kumweka katika kazi ya utumishi. Tunaweza kujifunza kwa baadhi ya watu ambao Mungu aliwaona ni waaminifu na kuwachagua na kuwafanya kuwa watumishi wa kazi yake, mfano wa Yesu, Musa na Paulo “....Yesu aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu. Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi....” Ebr 3:1,5. Mtume Paulo alikuwa ni mwaminifu ndio maana ameandika akisema, “Namshukuru Kristo Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake.” 1Tim 1:12.
- Yampasayo mtu ili aweze kudumu katika uaminifu.
- Bwana wetu Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani kwa sababu alikuwa ni mwaminifu kila alipojaribiwa na alizitambua hila za shetani wala hakufanya kosa lolote. Ndio maana ulipokaribia wakati wa kukamatwa aliwaambia wanafunzi wake akisema, “....yuaja mkuu wa ulimwengu huu hana kitu kwangu.” Yn 14:30.
- Kwa mkristo ambaye ameokoka, amejazwa Roho mtakatifu na kudumu katika uaminifu, Roho mtakatifu humfunulia hila zote za Shetani anapojaribiwa. Waliosimama imara katika neno la Mungu Shetani huja na kuwajaribu katika shida na dhiki. Usikubali mawazo ya shetani, bali mpinge na kumkemea, kwa kumwambia, nenda zako Shetani. “Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani,....Kisha Ibilisi akamwacha....” Mt 4:10-11. “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia, Mkaribieni Mungu naye atawakaribia ninyi....” Yak 4:7-8. Kutokana na andiko hili mtu anaweza kuwa karibu na Mungu na kumkemea Shetani naye huondoka, ikiwa analitii neno na kuishi linavyosema.
- Wale wote waliozaliwa mara ya pili imewapasa kuushinda ulimwengu na dhiki kwa sababu aliye ndani yao ni mkuu kuliko shetani, naye Yesu alimshinda na kushuhudia akisema, “Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.” Yn 16:33. Kwa upande mwingine, tunapolifahamu neno la Mungu tunazitambua hila za shetani na kumshinda. “Nao wakamshinda kwa damu ya mwana-kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao, ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.” Ufu 12:11. “....Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima....Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili (Jehanum).” Ufu 2:11-11.
- Kinachotokea kwa mtu anayedumu katika uaminifu.
- 1. Mungu humbariki na uzao wake. “Mtu mwaminifu atakuwa na Baraka tele” Mit 28:20.
- “Mwenye haki aendaye katika unyofu (uaminifu) wake, Watoto wake wabarikiwa baada yake.” Mit 20:7.
- 2. Mungu anakuwa pamoja naye. “Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.” Zab 145:18.
- 3. Anampendeza Mungu. “Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza.” Mit 11:20.
Utakatifu - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. " "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa, "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu" Walawi 19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema; “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...
Mungu awabariki lakini pia naomba somo la utii
JibuFutaMbarikiwe sana nimejifunza na kuna mahali nimevuka
JibuFutaNikweli Familia,Jamii,Selikali,KANISA nahata Mungu mwenyewe anamtafta mtu mwaminifu amuwakilishe Duniani
JibuFutaNahisi kubarikiwa amina
JibuFutaAmeni ameni hakika nimejifunza mambo mengi
JibuFutaHakika nabarikiwa sana
JibuFutaNaitaiji maombi zaidi asante nimemshinda shetani
FutaHakika mmekuwa chanzo Cha utakatifu kwangu
JibuFutaAmeeen god blessed you
JibuFutaAmina nimejifunza kitu
JibuFutaMungu awabariki sana nimejifunza mambo mengi sana pia nimebarikiwa mno Amen 🙏
JibuFutaAMINA
JibuFuta