Chanzo cha magonjwa.
Kuna magonjwa yanayotokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu
alipomponya yule mtu ambaye aliyekuwa mngonjwa akamwabia, “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi
tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi” Yn 5:14.
Ikiwa mtu aliyeokoka akirudia kuishi maisha ya dhambi pepo mchafu anapoona nafasi anachukua pepo wengine na kuingia kwake. Yesu alisema, “Mara huenda akachukua pamoja naye pepo wengine walio waovu kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa
humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa
kwa kizazi hiki kilicho kibaya” Mt 12:45.
Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni
matokeo ya ugonjwa katika mwili. Kwa upande mwingine mtu anaweza akawa ni mgonjwa au amekosa lishe.
Uponyaji wa Mungu.
Mambo ya kuzingatia na kuponywa ni haya yafuatayo;
1.kutubu na kuziacha dhambi.
Imeandikwa,
“Azifichaye
dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha on atapata rehema” Mithali 28:13. Pia andiko linasema, “Twajua ya kwamba Mungu
hawasikii wenye dhambi;bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake
huyo humsikia” Yhana 9:31.
2. Kuishi maisha ya utakatifu
Ndio maana Mungu amesema; “Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu
hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na
rehema aliyowaapia baba zako. Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote…” Kumb 7:12,
15. Katika maandiko haya tunaona Mungu alisema
na baba zetu. Pia katika nyakati hizi anasema nasi katika ahadi ya maandiko hayo yakwamba tunapozishika na kuzitenda hukumu zake
(Sheria zake). Naye hutuondolea ugonjwa wote. Kwa
sababu Mungu aliwaapia baba zetu ni ili kuthibitisha atafanya yale aliyoahidi. Kwa hiyo katika maisha yako yote yakupasa kumtegemea Mungu kwa yale yote aliyoahidi katika neno lake.
3.Kumwamini
Mungu na neno lake.
Ndiyo maana
Mungu alisema “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani;
Naye akisita-sita roho yangu haina furaha naye.” Ebr10:38.
Kutokana na andiko hili, linaonyesha
lazima mtu awe mwenye haki ndipo aweze kuishi kwa imani. Pia lazima kwanza
kuamini moyoni na kuwa na uhakika Mungu atakuponya kama neno linavyosema,“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo
yatarajiwayo, ni bayana (wazi) ya mambo yasiyoonekana” Ebr 11:1
Kwa sababu hiyo katika maisha yako yote yakupasa kumtegemea Mungu kwa yale yote aliyoahidi katika neno lake.
"Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote,…Mche Bwana, ukajiepushe na uovu, Itakuwa afya mwilini pako. Na mafuta mifupani mwako. Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzishike kauli zangu. Kwa maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote”Mit 3:5,7,8. 4. Kuishi maisha ya unyenyekevu.
“Dhabihu za Mungu ni mioyo iliyovunjika;
Moyo uliovunjika na kupondeka Ee Mungu hutaudharau. “Huwaponya waliopondeka
moyo, Na kuwaganga jeraha
zao” Zab 51:17; 147:3. Mungu anahitaji watu waliovunjika na kupondeka moyo ili
awaponye. Maana ya kuvunjika na kupondeka moyo ni kunyenyekea chini ya Mungu na
kujua yeye ni mwenye uwezo
na nguvu zote. Pia kunyenyekea ni kuacha kuwa na kiburi na kujiona wewe ni bora kuliko wengine,
kutokuonea na kunyanyasa wengine, kutokujivunia ulivyo nayo, na kujisifia kwa
yale unayoyafanya, kutokudharau
wengine na kuwapuuza. Andiko linasema “Amdharauye mwenzake afanya dhambi;…” Mit 14:21. Yesu Kristo yeye ni mfano kwetu, alikuwa ni mnyenyekevu
aliacha enzi na mamlaka aliyokuwa nayo mbinguni akaja duniani kwa namna ya
mtumwa hakutaka makuu na fahari, alimtii Mungu.
5. Kuomba kwa imani.
“Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya
kuwa , tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba
atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba”Yoh 5:14-15. Haya maandiko yanafundisha
ni muhimu kujua kwamba tunapomwomba Mungu anatuskia, tunapoomba sawaswa na
mapenzi yake (neno lake). Pia kujua
tulichoomba tunacho tayari. Kama umemwomba Mungu uponyaji unajua umekuponya. Hiyo ndiyo imani katika Mungu. Ndiyo maana Yesu
alifundisha akisema, “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaoombayo mkisali, aminini ya kwamba
mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” Mk 11:24.
6. Kuomba kwa bidii.
Kuomba
kwa bidii bila kukata tamaa naye Bwana atakuponye kabisa. Iwapo umeomba lakini
bado Bwana hajakuponya endelea kunyenyeke na kumlilia tena na tena mpaka Bwana akuponye. Kuna mifano ya watumishi wa Mungu maandiko waliomwomba Mungu kwa bidii tena na tena wakajibiwa. Mmojapo ni Eliya;
“Naye Eliya
akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi;
akainama uso mpaka magotini. Akamwambia mtumishi wake, kwea sasa ukatazame
upande wa bahari. Akakwea na kutazama, akasema, hakuna kitu. Naye akanena, enenda tena mara saba. Ikawa
mara ya saba akasema, tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama
mkono wa mtu. … Ikawa muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo,
ikawa mvua nyingi…” 1Fal
18:42-45. Hapa
maandiko yanaonyesha jinsi Eliya alimwomba Mungu mara ya kwanza na mara ya
pili, wingu la mvua halikutokea lakini hakukata tamaa aliendelea kuomba mpaka
mara ya saba wingu likaonekana na mvua ikanyesha.
Na mwingine aliyeomba kwa
bidii na kujibiwa ni Elisha baada ya kumtuma Gehazi mtumishi wake kumfufua
mtoto.
“Na Gehazi
akawatagulia, akaiweka ile fimbo juu ya mtoto; lakini hapakuwa na sauti wala
majibu. Basi Elisha
alipofika nyumbani, tazama, mtoto amekwisha kufa, amelazwa kitandani pake. Basi
akaingia ndani akajifungia mlango, yeye na Yule mtoto wote wawili, akamwomba
Bwana... Kisha akarudi, akatembea nyumbani, huko Na huko mara moja; akapanda
akajinyoosha juu yake; Na Yule mtoto akapiga chafya mara Saba, Na mtoto
akafumbua macho yake.” 2 Fal 4:31-35. Elisha naye
alimtuma mtumishi wake Gehazi akaiweke fimbo juu mtoto abaye alikuwa amekufa
ili afufuke, wala hakufufuka, lakini Elisha hakukata tamaa alikwenda mwenyewe
akamwomba Mungu mara ya kwanza na mara ya pili na mtoto akafufuka.
7. Kumshukuru Mungu.
“Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo
ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” 1The 5:18. Katika maisha yetu ni muhimu
tumshukuru Mungu kwa ajili ya mema yote anayotutende kila siku. Kwa Kufanya hivyo ni kutimiza agizo la Mungu kuhusu kushukuru.
Mungu ni mwaminifu kwako.
Usiogope kwa sababu yale yote aliyoyaahidi katika neno lake hakika atayafanya kama alivyosema; “Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili
Neno lililotoka midomoni mwangu.” Zab 89:34. “Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri
zangu” Kut 20:6. “Maana Kama vile mvua ishukavyo, Na theluji, kutoka mbinguni,
wala hairudi huko; Bali huinywesha ardhi, Na kuizalisha Na kuichipuza, ikampa
mtu apandaye mbegu, Na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu,
litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure Bali litatimiza mapenzi
yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma” Isa 55:10-11.
USHUHUDA.
Hapa ninatoa ushuhuda wa mtu
ambaye Bwana amemponya mara nyingi kwa magonjwa tofauti. Siri ya uponyaji wake
ni kwamba yeye ni mtakatifu amejilinda na kuepuka dhambi.
Amekuwa ni mwenye imani na unyenyekevu,
amevunjika na kupondeka moyo. Wakati mwingine anapomwomba Mungu huanguka
kifulifuli akimsihi Mungu. Hakika mtu kama huyu atasikilizwa kwa sababu anao
ujasiri mbele za Mungu, na ndani ya moyo wake hakuna dhambi inayomhukumu.
Ndio maana imeandikwa “Basi na tukikaribie
kiti cha neema kwa ujasiri ili tupewe
rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Ebr 4:16. Mtu anapodumu katika maisha
ya kumpendeza Mungu anapata
neema au upendeleo kujibiwa maombi. Wakati
mwingine hata kabla ya
kuomba hujibiwa. Andiko linasema “Na itakuwa
kwamba, kabla ya kuomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.” Isa 65:24. “….maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi
hamjamwomba.” Mt 6:8.
Mimi naitwa benedicta napatikana mkoani arusha na shida na magonjwa naombeni imani na maombi yenu
JibuFutaUbarikiwe sana mtumishi Wa Mungu
JibuFutaBarikiwa mtumishi
JibuFuta