Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUJAZWA ROHO MTAKATIFU

Hii ni ahadi ya Mungu kwa ajili ya watu wote.

Kwa sababu hiyo kila aaminiye atajazwa Roho Mtakatifu.Mungu aliahidi kwa kinywa cha nabii Yoeli wakati wa agano la kale akasema,“Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono, tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile nitamimina roho yangu” Yoeli 2:28,29.

Pia katika agano jipya maandiko yanathibitisha ya kwamba kila anayemwamini Yesu atajazwa Roho Mtakatifu.


Mitume na wale wengine waliokuwa pamoja nao.

Matendo ya Mitume 2:4, 11

4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.


Kutokana na hili andiko hapa juu wote walijazwa ni wale waliokuwa wamesubiri ahadi ya Roho Mtakatifu, ambao idadi yao imetajwa katika,

Matendo ya Mitume 1:15  Siku zile akasimama Petro kati ya hao ndugu (jumla ya majina ilipata mia na ishirini);


Yesu amethibitisha kwa wale wote wamwaminio watajazwa Roho Mtakatifu.

Marko 16:17  Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;


Yohana 7:38-39

38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.


39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.


Wanafunzi waliomwamini Yesu huko Efeso wote walijazwa Roho Mtakatifu.

Matendo ya Mitume 19:2, 6-7

2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.


6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.


7 Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.


Huko Kaisaria Kornolio na watu wote walikusanyika walijazwa Roho Mtakatifu. Ni wakati Petro alipokuwa anawaambia maneno ya Mungu.

Matendo ya Mitume 10:44  Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.


Huko Korintho na Efeso Paulo alifundisha kama ifuatayo;

Waefeso 5:18  Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;


1 Wakorintho 14:5  Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.


Kutokana na mistari hiyo neno mjazwa Roho na  mnene kwa lugha, yanaonyesha wingi.

Kwa sababu hiyo inamaanisha ya kwamba watu wote wajazwe Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha.


Ni nani atampokea Roho Mtakatifu?

1) Anayetubu na kusamehewa.

Matendo 2:38. 

 akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu” 


2) Anayemtii Mungu. 

Matendo 5:32.

Anayemtii Mungu ni mtu yule aliyemwamini  Yesu na kuishi sawasawa na neno la Mungu.

“Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio” 


3) Aliye na kiu na kumwamini Yesu. 

Yohana 7:37-39.

“…Yesu akasimama; akapaza sauti yake akasema, mtu akiona kiu (kutamani), na aje anywe. Aniaminiye, kama vile maandiko yanavyonena, mito ya maji yalio hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminiye watampokea badaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa” 


4) Anayekubali ubatizo wa maji mengi. Anatimiza haki.

 Ni jambo la muhimu kufahamu ya kwamba ubatizo sahihi ni ule ambao Mungu alimwagiza Yohana hata akambatiza Yesu ili kutimiza majawapo ya agizo la Mungu. 


Ndio maana imeandikwa kwenye 

“MATHAYO 3:15 - Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.”


Anayepinga.

- Haiwezekani kwa mtu ambaye anampinga Mungu kuhusu ubatizo halisi wa maji mengi, halafu akampokea Roho Mtakatifu. 


Kuzaliwa kwa maji na Roho.

Ni jambo la Muhimu. 

Yohana 3:5-6.

“Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.


Maana ya kuzaliwa kwa maji na Roho.

1. Kuzaliwa kwa maji ni wakati mtu anapobatizwa kwa​ kuzamishwa ndani ya maji mengi. 


2. Pia mtu huzaliwa kwa Roho wakati ameamua kuokoka na  kumwamini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake kwa kutubu na kuziacha dhambi.  


Ni wakati gani mtu anajazwa Roho Mtakatifu?

1). Mtu anajazwa Roho Mtakatifu wakati anapofanya ibada.

'MATENDO 4:31  Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.'


- Pia mtu anaweza kujazwa Roho Mtakatifu akiwa anaomba ananwabudu na kumsifu Mungu. Au wakati anapobatizwa.


- Inampasa aaminiye kuishi maisha ya utakatifu kwa kuwa Roho Mtakatifu yeye ni Mtakatifu, hukaa na wale walio watakatifu.


Kinachotokea aaminiye anapojazwa Roho Mtakatifu.

 1). Anapokea nguvu

Matendo 1:8, 4:31

“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.…wote wakajaa Roho mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri” 


2). Roho Mtakatifu anakaa ndani ya aaminiye.

Yohana 14:17.

Yesu alisema, “Ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala kumtambua; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu” 


3). Anasema kwa lugha  nyingine..

Anakuwa amejaliwa kusema kwa lugha nyingine.

Matendo 2:4.“Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka” 


Ni kwa nini Roho Mtakatifu alikuja kwetu? Majibu ya swali hili ni kama ifuatavyo:

1)Alikuja ili kukaa nasi na kutusaidia.

Yesu alisema, “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele. Ndiye Roho wa kweli…”Yohana 14:16, 17. 


2). Kutusaidia kuomba.

Warumi 8:26,

“Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu” 


3). Kutuongoza na kutuambia mambo yajayo.

Yesu alisema, “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatoa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu, kwa hiyo nalisema ya kwamba atatoa yaliyo yangu na kuwapashani habari” Yohana 16:13-15.


- Sharti huwaongoza wale ambao ni watoto wa Mungu.

 “Kwa kuwa wote wanaongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” Warumi 8:14.


4). Kutufundisha na kutukumbusha.

Yesu alisema,“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” Yohana 14:26.


5). Kutumiminia pendo la Mungu.

“ na tumaini halitahayarishi, kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu aliyetupa sisi” Warumi 5:5.

 

6) Anatupa furaha.

“1 WATHESALONIKE 1:6 - ⓔ Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu.”

“MATENDO 13:52 - Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.”


7). Kuuhakikishia ulimwengu    

Yesu alisema,“…huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu” Yohana 16:7,8.  


Roho Mtakatifu anauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu kupitia watumishi wa Mungu wanapohubiri na kufundisha neno la Mungu.


8) Kutushuhudia kuwa watoto wa Mungu. 

Warumi 8:16.

“lRoho mwenyewe hutushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu.”


- Anayeshuhudiwa ni yule mtu ambaye amefanyika kuwa mtoto wa Mungu.

Yohana 1:12  Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;


Asiye Na Roho Mtakatifu Hukataliwa.

'WARUMI 8:9 - Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.'


Endelea kusoma zaidi,;

Uthibitisho kujazwa Roho Mtakatifu



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII

Kutokana na kichwa cha somo hapo juu mkristo ataweza kumtumikia Mungu kwa bidii kama ataweka nia katika  moyo wake.   Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa Roho Mtakatifu. Lakini hakuweza kuniombea, bali alipojibu ya kwamba nimwombe ...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...

UPONYAJI WA MAGONJWA.

Chanzo cha magonjwa. Kuna magonjwa yanayotokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya yule mtu ambaye aliyekuwa mngonjwa akamwabia,   “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi”   Yn 5:14.   Ikiwa mtu aliyeokoka akirudia kuishi maisha ya dhambi pepo mchafu anapoona nafasi anachukua pepo wengine na kuingia kwake. Yesu alisema,  “Mara huenda akachukua pamoja naye    pepo    wengine walio waovu    kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”   Mt 12:45.    Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili. Kwa upande mwingine mtu anaweza akawa ni mgonjwa au amekosa lishe.  Uponyaji wa Mungu.                     Mambo ya kuzingatia na kuponywa ni ha...