Ruka hadi kwenye maudhui makuu

HEKALU LA MUNGU

 Maana ya hekalu katika Biblia

A. Hekalu ni nyumba ya ibada. Ni kama ile nyumba Sulemani aliyomjenngea Mungu. 1 Wafalme 6:14

Basi Sulemani akaijenga hiyo nyumba akaimaliza.


B. Hekalu ni mahali patakatifu panapohusishwa na ibada na uwepo wa Mungu. Uthibitisho wa jambo hilli unapatikana kwenye, 2 Mambo ya Nyakati 5:13-14

13 hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana,


14 hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana.


Kila aaminiye ni hekalu la Mungu.

Inawezekana kuwa hekalu la Mungu kwa kuzingatia haya yafuatayo;

1. Amempokea Yesu na kuokolewa kutoka katika dhambi zake zote. Na kuziacha kabisa.

2.  Anaishi sawasawa na maneno ya Mungu.

3. Anadumu katika maisha ya utakatifu. 


4. Anatoa mwili wake kama sadaka na hekalu la Mungu akiwa amefanywa upya. Ndio maana imeandikwa katika Warumi 12:1-2

1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.


2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


1 Petro 2:5  Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.


Kulingana na maandiko hapa juu yanaonyesha aaminiye anapaswa kutoa mwili na roho yake kuwa dhabihu kwa Mungu. Jambo hilli linawezekana kwake ikiwa anao uhusiano mzuri na Mungu.


Hekalu ni mahali ambapo panapaswa kuwa patakatifu. Kwa hiyo Mungu hukaa kwenye hekalu takatifu. Imeandaliwa kwenye,

 1 Wakorintho 3:16-17

16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?


17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.


'1 WAKORINTHO 6:19 - ‘Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu Wala ninyi si mali yenu wenyewe’


'WAEFESO 2:22 - ‘Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.' (Neno maskani linamaanisha makao au mahali pa kukaa).


Aaminiye kumkaribia Mungu katika Roho Mtakatifu.

1. Imeandikwa kwenye huu mstari hapa chini unasema “kwa yeye” (yaani Yesu Kristo). Ina maana katika Yesu Kristo tunamkaribia Baba katika Roho.

'WAEFESO 2:18 Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja.'

Yohana 4:24  Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Kwa sababu hiyo kulingana na maandiko hapa juu yanaonyesha umuhimu wa kuwa na Roho Mtakatifu.


Aaminiye Kumkaribia Mungu kwa Imani.

2. “WAEFESO 3:12  Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.”


Kwenye huu mstari neno ‘katika yeye’ linamaanisha Yesu. Kwa hiyo katika Yesu tunao ujasiri na uwezo kumkaribia Mungu na kumtegemea kwa imani 


Pia tunaweza kuona aliye na ujasir ni yule ambaye ameokolewa. Na pia anaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu na kuepuka

dhambi. Huyo anao ujasiri. Ndio maana imeandikwa kwenye,

'1 YOHANA 3:21 - 22 

21 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu'


22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.’



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII

Kutokana na kichwa cha somo hapo juu mkristo ataweza kumtumikia Mungu kwa bidii kama ataweka nia katika  moyo wake.   Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa Roho Mtakatifu. Lakini hakuweza kuniombea, bali alipojibu ya kwamba nimwombe ...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...

UPONYAJI WA MAGONJWA.

Chanzo cha magonjwa. Kuna magonjwa yanayotokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya yule mtu ambaye aliyekuwa mngonjwa akamwabia,   “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi”   Yn 5:14.   Ikiwa mtu aliyeokoka akirudia kuishi maisha ya dhambi pepo mchafu anapoona nafasi anachukua pepo wengine na kuingia kwake. Yesu alisema,  “Mara huenda akachukua pamoja naye    pepo    wengine walio waovu    kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”   Mt 12:45.    Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili. Kwa upande mwingine mtu anaweza akawa ni mgonjwa au amekosa lishe.  Uponyaji wa Mungu.                     Mambo ya kuzingatia na kuponywa ni ha...