Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KULEA WATOTO KATIKA MAADILI 2

Tunaweza kuendelea na somo hili sehemu ya pili kuhusu kuwalea watoto. Ni muhimu kwanza kufahamu mtoto anayo hisia.Ndio maana mtoto anapozaliwa anahisi mazingira tofauti ya hapa duniani. 

Mojawapo ya mambo ambayo yanadhihirisha wazi ya kwamba anayo hisia au kuhisi ni haya yafuatayo:

1. Mama yake anapomwekea ziwa mdomoni kwa mara ya kwanza azaliwapo huanza kunyonya.

2. Wakati akiwa ni mwenye njaa hulia kwa sababu anahisi njaa.

3. Wakati anapoumwa au kuumia hulia kwa sababu anahisi maumivu. 

4. Wakati wa baridi au joto kali anakuwa anahisi. Ndio maana mtoto akiwa analia sana ujue kuna sababu. Chunguza ni kwa nini analia ili upate ufumbuzi na kumsaidia. Wakati mwingine inawezekana hakupata usingizi wa kutosha anao uchovu. Pia kutokana na mazingira mnayoishi kuna usumbufu wa kelele za mara kwa mara. Kwa sababu hiyo hawezi kupata usingizi. 

5. Mama anapomlaza mtoto na kumwacha anahisi yuko pekee yake na hatimaye kulia.

Baada ya mtoto kuzaliwa hujifunza mambo mbalimbali.Jambo mojawapo mtoto hujifunza ni kuongea. Ni pale anapowasikia wazazi au walezi maneno wanayosema ndipo na yeye anaanza kusema neno mojawapo ambalo amewahi kulisikia.

Kwa hiyo kwa kadri anavyoendelea kukua unafika wakati ambao anaanza kuunganisha maneno na kuyasema kwa usahihi.

Pia hujifunza na kuiga kila kitu anachosikia na anachokiona kwa mtu yeyote kama katika familia, watoto wenzake na watu wengine.

 Kwa sababu hiyo ni muhimu  kumlinda na kuhakikisha watu anaokaa nao katika familia ni salama. Na pia wawe ni watu wanaomjenga katika misingi ya maadili mema. 

Ili kumjenga katika maadili mema. Mfundishe mtoto katika maadili haya yafuatayo;

> Kumshukuru Mungu kwa ajili ya chakula kabla ya kula.

> Kufanya ibada mbele za Mungu kwa kuomba, kusifu na kuabudu.

> Kuwaheshimu watu ambao wamemzidi umri na kuwaamkia. Pia kuwaheshimu watoto wenzake ambao wanalingana umri. 

Katazo au onyo kwa mtoto.Kumkataza mtoto kwa yale mambo ambayo hayafai na kumwambia acha hiyo siyo njia pekee ya kumjenga.

Ikiwa mtoto anazungumza maneno mabaya ambayo alisikia ni muhimu kwa mzazi au mlezi kumrekebisha na kumwambia maneno hayo ni mabaya usiyaseme tena, hayafai, na wala hayampendezi Mungu. Na hatimaye huacha kuyasema na kuweka kumbukumbu moyoni mwake ya kwamba hayo ni maneno mabaya hayafai kusemwa.  

Mtoto akishafikisha umri wa miaka mitatu ni mwepesi kutaka kujua kila kitu anchokiona ni nini? Au kinaitwaje? Kwa hiyo anapokuwa amefikia umri huo wakati unaendelea kumlea katika neno la Mungu na kushiriki naye katika ibada atakuwa mcha Mungu na mnyenyekevu. Na baadhi yao walio na umri huo wamejaliwa na Mungu kujazwa Roho Mtakatifu na kunene kwa lugha mpya. 

Kumchapa mtoto siyo njia pekee ya kumrekebisha kwa sababu yamkini hajui kosa alilofanya. Kwa sababu hiyo kabla ya kumchapa mtoto ni muhimu kumfahamisha kosa lake ili aweze kulifahamu. Kwa kufanya hivyo anakuwa amelifahamu kosa lake na kujirekebisha. Kumchapa mtoto ni hatua inayofuata baada ya kumwambia kosa lake. Kuwa makini usimchape mtoto wako wakati unayo hasira kwa sababu hutakiwa na busara na hatimaye utamuumiza. 

Angalizo au tahadhari. Kuwa makini sana wewe mzazi na mlezi. Kwa sababu watoto hujifunnza kile wanachokiona au kusikia. Kwa ajili ya malezi mema ni muhimu kuvaa mavazi ya staha ambayo yanasitiri mwili. Jambo lingine la muhimu epuka ugomvi na mabishano mbele ya watoto. 

Malezi ya mtoto huanzia nyumbani. Shule ya kwanza ya mtoto inaanza nyumbani kwa wazazi wake. Kwa hiyo wazazi wanapaswa kuwalea watoto wao katika maadili mema na kuwalinda au kuwaepusha na mabaya. Wewe mzazi au mlezi ndiwe mlinzi wa mtoto. Hakikisha mtoto wako yuko salama wakati wote. Soma sehemu ya kwanza


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII

Kutokana na kichwa cha somo hapo juu mkristo ataweza kumtumikia Mungu kwa bidii kama ataweka nia katika  moyo wake.   Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa Roho Mtakatifu. Lakini hakuweza kuniombea, bali alipojibu ya kwamba nimwombe ...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...

UPONYAJI WA MAGONJWA.

Chanzo cha magonjwa. Kuna magonjwa yanayotokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya yule mtu ambaye aliyekuwa mngonjwa akamwabia,   “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi”   Yn 5:14.   Ikiwa mtu aliyeokoka akirudia kuishi maisha ya dhambi pepo mchafu anapoona nafasi anachukua pepo wengine na kuingia kwake. Yesu alisema,  “Mara huenda akachukua pamoja naye    pepo    wengine walio waovu    kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”   Mt 12:45.    Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili. Kwa upande mwingine mtu anaweza akawa ni mgonjwa au amekosa lishe.  Uponyaji wa Mungu.                     Mambo ya kuzingatia na kuponywa ni ha...