Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UPENDO WA KWANZA KUPOA.

Namshukuru Mungu kwa ajili ya wakati huu ambao amenijalia kuutumia kuandika somo hili ambalo linahusu upendo wa kwanza kupoa. Ili uweze kufahamu nitaeleza kwa uhalisi ya kwamba mtu anapokuwa ameokoka anakuwa na hamasa ndani ya moyo wake, au kwa maneno mengine naweza kusema anakuwa na shauku, kiu na hamu kwa ajili ya mambo ya Mungu. Huo ndio upendo wa kwanza. Mtu wa namna hiyo inaonesha wazi anampenda Mungu. Kwa sababu hiyo anakuwa na bidii ya kujifunza neno la Mungu, na kuutafuta uso wa Mungu kwa maomba, kumwabudu na kumsifu kila wakati. Kuwa hiyo ikiwa Mkristo aliyeokoka anafanya hayo anakuwa amedumu katika ule upendo wa kwanza.

Kuacha upendo wa kwanza.
Mkristo ambaye ameokoka yampasa kuwa makini asije akaacha kuwa na upendo wa kwanza kwa ajili ya shughuli za dunia na udanganyifu wa yule mwovu. Hapa nitaonesha mambo ambayo ni sababu ya mtu kuacha upendo wa kwanza ambazo ni kama ifuatavyo;


1. Kufanya dhambi au kuishi katika dhambi. 

2.Shughuli za dunia hii. Kutokana na shughuli za kila siku mtu anakuwa hana muda wa kumtafuta Mungu. Kwa hiyo Mtu anapotumia muda mwingi katika mambo yake bila kuutafuta uso wa Mungu anakuwa ameuacha upendo wa kwanza.

3.Kutumia mitandao bila kuwa na kiasi.
Kama mtu atakuwa anatumia mitandao ya intaneti bila kuwa na kiasi cha muda wa kikomo anaweza kutumia muda mwingi zaidi kuliko kuwa na muda wa kutosha kumtafuta Mungu. Kwa sababu hiyo ni muhimu kutumia mitandao ya kijamii kwa kiasi, ambayo ni Facebook, WhatsAp na Instagram. Hii ni baadhi ya mitandao michache nimeitaja hapa. Jambo lingine ambalo ni kinyume na  Mungu haiwezekani ukaipenda mitandao na mambo mengine na kujishughulisha nayo kuliko Mungu. Katika maisha yetu jambo la muhimu ni kumpa Mungu nafasi ya kwanza. Na pia katika jambo lolote kabla ya  kulifanya yakupasa kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yako. Kwa hiyo Kila siku asubuhi mtu anapoamka  kabla ya kufanya shughuli yoyote ni jambo la muhimu kumpa Mungu nafasi ya kwanza kwa kufanya ibada. Mtumishi wa Mungu Paulo alikuwa anafahamu ya kwamba hilo ni jambo la muhimu kabla ya mambo yote. Ndio maana aliagiza na kusema; “Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu” Timotheo 2:1-2.

Kutokana na andiko hili hapa juu yakupasa kufanya dua, sala, maombezi na shukrani kama ifuatavyo;
A.Kuomba kwa ajili yako na kwa ajili ya familia yako.
B.Kuomba kwa ajili mambo yote ili Mungu akusaidie na kukuongoza. “Nafsi zetu zinamngoja BWANA; Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu”. Zaburi 33:20. “Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.” Isaya 58:11.
C.Kuomba  kwa ajili ya wengine.
D.Kumshukuru Mungu kwa ajili ya mambo yote  ambayo umeomba kwake. "Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu". 1 Wathesalonike 5:18. 

aliyemwamini Yesu na kuzaliwa mara ya pili ni muhimu kufahamu ya kwamba yampasa kuomba katika mapenzi ya Mungu. Ina maana kuomba kulingana na neno la Mungu. Hapa nitatoa mfano wa mtu anayeomba vibaya na kinyume neno la Mungu. Ni pale mtu ambaye ni mwizi anaomba Mungu amfanikishe kuiba fedha ya mtu mwingine.

Matokeo ya mtu kupoa na kutokuwa  na upendo wa kwanza ni haya yafuatayo;
1. Mtu ambaye amepoa anapoteza uhusiano wake wa kuwa karibu na Mungu katika maisha yake. Pia anakuwa amepoteza hofu ya Mungu.

2. Anakuwa hajali mambo ya Mungu, bali anajali mambo yake zaidi kuliko ya Mungu. Mtu wa namna hiyo anakuwa ameyazoea mambo ya Mungu. Ndani ya moyo wake hana unyenyekevu wala kupondeka.

3. Anakuwa hana ile shauku au hamu ya kupenda mambo ya Mungu  kama kuomba na kusoma neno la Mungu.

Kujifunza zaidi bofya hapa; dua, sala na maombezi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...

UPONYAJI WA MAGONJWA.

Chanzo cha magonjwa. Kuna magonjwa yanayotokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya yule mtu ambaye aliyekuwa mngonjwa akamwabia,   “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi”   Yn 5:14.   Ikiwa mtu aliyeokoka akirudia kuishi maisha ya dhambi pepo mchafu anapoona nafasi anachukua pepo wengine na kuingia kwake. Yesu alisema,  “Mara huenda akachukua pamoja naye    pepo    wengine walio waovu    kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”   Mt 12:45.    Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili. Kwa upande mwingine mtu anaweza akawa ni mgonjwa au amekosa lishe.  Uponyaji wa Mungu.                     Mambo ya kuzingatia na kuponywa ni ha...

KUWEKWA HURU KUTOKA DHAMBI YA UZINZI NA UASHARATI.

Jambo la kwanza ninamshukuru Mungu kwa neema yake aliyonipa kufundisha neno lake. Ndungu mpendwa ninajua ya kwamba Mungu alikupenda sana, hata akamtoa Mwana wake wa pekee Yesu Kristo kwa ajili yako ili akukomboe kutoka katika dhambi zote ikiwemo dhambi ya uzinzi na uasherati. Sasa ninakusihi kwa neema ya Mungu fuatana nami kwa makini kuhusu  somo hili nawe utauna utukufu wa Mungu katika maisha yako. Tunaweza kuangalia kwa makini dhambi ya uzinzi na uasharati ambayo mtu akiitenda inaharibu ufahamu wake na hatimaye kuangamia. Mtu anapoteza uhusiano wake na Mungu, mawasiliano kati yake na Mungu yanakatika. Mungu  ni Makatifu hana ushirika na wenye dhambi. “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” Mithali 6:26.   “Lakini maovu yenu yamewafarikisha (yamewatenganisha) ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki  kusikia.”   Isahau 59:2. Atendaye dhambi ya zinaa au  uasherati ...

KUDUMU KATIKA UPENDO WA MUNGU.

Neno la Mungu katika Biblia linatufudisha kuhusu upendo wa Mungu  kwetu. Yeye Mungu ndiye  mwanzo wa upendo kwa sababu alitupenda kwanza. “...alitupenda sisi kwanza”.   1 Yohana 4:19. Jinsi mtu anavyoweza kuwa na upendo wa Mungu. Ni pale mtu anapokuwa amezingatia kudumu katika upendo wa Mungu kama ifuatavyo; 1.Kuishi sawasawa na maagizo yote ya neno la Mungu na kumpenda. “Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;”   Kumbukumbu la Torati 10:12.   “Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwaamuru, kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote”.   Yoshua 22:5. 2. Jambo lingine la kuzingatia ni kwamba yampasa mtu kuyashika maagiz...

MADHARA YA DHAMBI.

Huu ni wakati mwingine ambao Bwana amenijalia kuwepo kwa kusudi lake jema. Nitaelezea katika somo hili kuhusu dhambi ilivyo na madhara kwa mtu aitendaye. Kwanza tuangalie dhambi  ilivyoanza kwa Adamu na Hawa ni wakati walipokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo Mungu aliwakataza wasile. Kwa sababu hiyo dhambi ilisababisha madhara mengi kwa uzao wake na vizazi vyote duniani. Kwa hiyo shida zote zilizopo duniani zimetokana na dhambi. Kutokana na wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa kwa kuwa walitenda dhambi na vizazi vingine vyote vimehesabiwa ni wenye dhambi. Mtu  anazaliwa akiwa na asili ya dhambi kutoka kwa wazazi wa kwanza Adamu na Hawa. Warumi 3:23 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;” Kutokana na sababu hiyo ndio maana kila mwanadamu anakufa sawasawa na Mungu  alivyosema katika kitabu cha Mwanzo 2:16-17 “BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa u...