Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZURI.

Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu wengine, kwa sababu hakuna mtu anayejua kila kitu au kila jambo na anayeweza kufanya kila kitu mwenyewe hapa duniani. Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Kwa sababu hiyo ili mtu apate msaada wa wengine ni lazima ajue  namna ya kuishi na watu vizuri. Na ndipo ataishi kwa amani na watu wote. Zifuatazo ni kanuni muhimu za kuishi na watu. 

1. Kuwapenda watu wote bila kubagua. Kwa sababu watu wote chanzo chake ni Mungu aliwaumba. Yeye ni Baba wa wote. Kwa sababu hiyo kila mtu ametokana na Mungu.

2. Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana.


3. Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake, hata akiwa ni masikini, hakuelimika, hana cheo cha juu na kadhalika.

4. Uwe mtu wa furaha katika Mungu siku zote. Kwa kulisoma neno lake, kuomba na kumsifu.

5 Uwe mtu unayesimamia neno la Mungu linavyosema, wala usikubali kupotoshwa na mtu yeyote kwanda kinyume na neno la Mungu.

6. Usipende kulaumu watu. Kama kuna sababu ya kulaumu tumia njia nzuri ambayo ni kushauri kwa upole ili kumsaidia na kumjenga aliye kosea.

7. Usiwe msengenyaji kwa kumsema mtu vibaya. 

8. Usiwe mtu wa kuwagombeza wale wanaokosea bali uwaonye kwa upole. Wala usiwadhihaki na kuwachukia  bali yachukie maovu yao na kuyaepuka. Huku ukijilinda usije ukawa mkosaji kama wao.

9. Shukru kwa kila jambo jema unalofanyiwa kwa kusema ahsante au nashukuru.

10. Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu au wakubwa.

11. Usiwe mtu wa mabishano. Na kama ikitokea mtu anabishana na wewe usitake kushindana.

12. Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu. Huku ukichukuliana na adui zako kwa kuwasamehe, naye Mungu atakuwa upande wako na kukutetea.

13. Usiwe mtu wa kugombana, kupiga au kupigana na watu.

14. Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa lolote lile kama kuna jambo zuri kwako acha wengine wakusifu. Lakini ujue ya kwamba sifa zote anastahili Mungu aliyekuumba hata ukatenda jambo zuri.

15. Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki. Achilia na kusahau yale yote uliyokosewa na kuyasamehe, wala usiyakumbuke tena.

16. Usilipize kisasi, badala yake tenda wema kwa Yule anayekukosea. Mungu pekee ndiye alipaye kisasi. Ijapokuwa Mungu ndiye alipaye kisasi  hupaswi kuwatakia adui zako mabaya, wala kufurahia wanapopatwa na mabaya.

17. Usiwe unachonganisha watu. Kama ukiambiwa udhaifu wa mtu usiende kumwambia aliyesema.

18. Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako, ndipo na watu nao watakupenda na kukubali kama ulivyo.

19. Tunza siri zako na za wengine. Ni Muhimu kufahamu ya kwamba si kila mtu ukimwambia mambo yako ya siri atayatunza bila kuwaambia watu wengine. Kwa hiyo kuwa makini na kutambua ni nani anayeweza kukutunzia siri.

20. Usiwe mwepesi wa hasira. 

21. Kumbuka majina ya watu uliosomwa nao, na wale ambao mnafahamiana.

22. Usiwe mzungumzaji kupita kiasi, badala yake uwe msikilizaji mzuri.

23. Usiseme uongo au kuongeza chumvi au kupotosha ukweli.

24. Mazungumzo Yoyote baina yako na wengine yawe sawasawa neno la Mungu. Yakiwa kinyume na neno la Mungu yakatae na kuyaepuka.

25. Maliza ugomvi au migogoro na wengine kwa njia ya amani kwa kuzungumza na mhusika.

26. Jifunze kusamehe makosa ya watu na kuyasahau na  wala usiyakumbuke tena.

27. Unapofanya makosa, kubali na kuungama na kuomba msamaha.

28. Heshimu na kuvumilia 
mawazo na maoni ya watu wengine ambayo ni tofauti na yako.

Maoni

  1. 29. Epuka kwenda kwa mtu mala kwa mala mda wa mlo.

    JibuFuta
  2. Nashulu sana nimejifunza sana hapa ila bado naomba mungeongezea namna ya kujinasua na kuepukana na watu wabaya

    JibuFuta
  3. Bila jina15:31

    Somo zuri sana hili.
    Shukrani sana mwandishi!

    JibuFuta
  4. Bila jina19:47

    Muheshim kila m2 usimdharau kwa jins alivyo muonekano wake hat kama yupo katika mazingira magum nuheshim na mtie moyo asikate tamaa pia msaidie mbinu za kimaisha atakushukur sana 2 pi atakuombea kwa mng ufanikiwe zaid

    JibuFuta
  5. Bila jina22:55

    Mchapishahi tunashukuru Sana kwa ushauri nzuri Sana

    JibuFuta
  6. Bila jina16:55

    Barikiwa sana

    JibuFuta
  7. Bila jina15:08

    Asate sana

    JibuFuta
  8. Bila jina07:21

    Nashukulu San kwa somo zuri ila nilikuwa naomba mtuongezeee namna ya kumjua mtu mnafiki yaan anayejufanya anakupenda af badae anakusem vibaya kwa watu wengine

    JibuFuta
  9. Bila jina15:26

    Shukrani Sana nimefunguka Sana kweny Mambo mengi

    JibuFuta
  10. Bila jina23:58

    Thanks

    JibuFuta
  11. Bila jina19:20

    Asante sana nimefunguka sana kwenye mambo mengi

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...