Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu wengine, kwa sababu hakuna mtu anayejua kila kitu au kila jambo na anayeweza kufanya kila kitu mwenyewe hapa duniani. Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Kwa sababu hiyo ili mtu apate msaada wa wengine ni lazima ajue namna ya kuishi na watu vizuri. Na ndipo ataishi kwa amani na watu wote. Zifuatazo ni kanuni muhimu za kuishi na watu.
1. Kuwapenda watu wote bila kubagua. Kwa sababu watu wote chanzo chake ni Mungu aliwaumba. Yeye ni Baba wa wote. Kwa sababu hiyo kila mtu ametokana na Mungu.
2. Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana.
3. Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake, hata akiwa ni masikini, hakuelimika, hana cheo cha juu na kadhalika.
4. Uwe mtu wa furaha katika Mungu siku zote. Kwa kulisoma neno lake, kuomba na kumsifu.
1. Kuwapenda watu wote bila kubagua. Kwa sababu watu wote chanzo chake ni Mungu aliwaumba. Yeye ni Baba wa wote. Kwa sababu hiyo kila mtu ametokana na Mungu.
2. Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana.
3. Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake, hata akiwa ni masikini, hakuelimika, hana cheo cha juu na kadhalika.
4. Uwe mtu wa furaha katika Mungu siku zote. Kwa kulisoma neno lake, kuomba na kumsifu.
5 Uwe mtu unayesimamia neno la Mungu linavyosema, wala usikubali kupotoshwa na mtu yeyote kwanda kinyume na neno la Mungu.
6. Usipende kulaumu watu. Kama kuna sababu ya kulaumu tumia njia nzuri ambayo ni kushauri kwa upole ili kumsaidia na kumjenga aliye kosea.
7. Usiwe msengenyaji kwa kumsema mtu vibaya.
8. Usiwe mtu wa kuwagombeza wale wanaokosea bali uwaonye kwa upole. Wala usiwadhihaki na kuwachukia bali yachukie maovu yao na kuyaepuka. Huku ukijilinda usije ukawa mkosaji kama wao.
9. Shukru kwa kila jambo jema unalofanyiwa kwa kusema ahsante au nashukuru.
10. Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu au wakubwa.
11. Usiwe mtu wa mabishano. Na kama ikitokea mtu anabishana na wewe usitake kushindana.
12. Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu. Huku ukichukuliana na adui zako kwa kuwasamehe, naye Mungu atakuwa upande wako na kukutetea.
13. Usiwe mtu wa kugombana, kupiga au kupigana na watu.
14. Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa lolote lile kama kuna jambo zuri kwako acha wengine wakusifu. Lakini ujue ya kwamba sifa zote anastahili Mungu aliyekuumba hata ukatenda jambo zuri.
15. Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki. Achilia na kusahau yale yote uliyokosewa na kuyasamehe, wala usiyakumbuke tena.
16. Usilipize kisasi, badala yake tenda wema kwa Yule anayekukosea. Mungu pekee ndiye alipaye kisasi. Ijapokuwa Mungu ndiye alipaye kisasi hupaswi kuwatakia adui zako mabaya, wala kufurahia wanapopatwa na mabaya.
17. Usiwe unachonganisha watu. Kama ukiambiwa udhaifu wa mtu usiende kumwambia aliyesema.
18. Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako, ndipo na watu nao watakupenda na kukubali kama ulivyo.
19. Tunza siri zako na za wengine. Ni Muhimu kufahamu ya kwamba si kila mtu ukimwambia mambo yako ya siri atayatunza bila kuwaambia watu wengine. Kwa hiyo kuwa makini na kutambua ni nani anayeweza kukutunzia siri.
20. Usiwe mwepesi wa hasira.
21. Kumbuka majina ya watu uliosomwa nao, na wale ambao mnafahamiana.
22. Usiwe mzungumzaji kupita kiasi, badala yake uwe msikilizaji mzuri.
23. Usiseme uongo au kuongeza chumvi au kupotosha ukweli.
24. Mazungumzo Yoyote baina yako na wengine yawe sawasawa neno la Mungu. Yakiwa kinyume na neno la Mungu yakatae na kuyaepuka.
25. Maliza ugomvi au migogoro na wengine kwa njia ya amani kwa kuzungumza na mhusika.
26. Jifunze kusamehe makosa ya watu na kuyasahau na wala usiyakumbuke tena.
27. Unapofanya makosa, kubali na kuungama na kuomba msamaha.
28. Heshimu na kuvumilia
mawazo na maoni ya watu wengine ambayo ni tofauti na yako.
29. Epuka kwenda kwa mtu mala kwa mala mda wa mlo.
JibuFutaNashulu sana nimejifunza sana hapa ila bado naomba mungeongezea namna ya kujinasua na kuepukana na watu wabaya
JibuFutaSomo zuri sana hili.
JibuFutaShukrani sana mwandishi!
Muheshim kila m2 usimdharau kwa jins alivyo muonekano wake hat kama yupo katika mazingira magum nuheshim na mtie moyo asikate tamaa pia msaidie mbinu za kimaisha atakushukur sana 2 pi atakuombea kwa mng ufanikiwe zaid
JibuFutaMchapishahi tunashukuru Sana kwa ushauri nzuri Sana
JibuFutaBarikiwa sana
JibuFutaAsate sana
JibuFutaNashukulu San kwa somo zuri ila nilikuwa naomba mtuongezeee namna ya kumjua mtu mnafiki yaan anayejufanya anakupenda af badae anakusem vibaya kwa watu wengine
JibuFutaShukrani Sana nimefunguka Sana kweny Mambo mengi
JibuFutaThanks
JibuFutaAsante sana nimefunguka sana kwenye mambo mengi
JibuFuta