Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TUNDA LA KIASI.

Maana ya neno kiasi ni kujitawala. Neno kiasi linatokana na neno la  Kiyunani  (enkrateia) ambalo maana yake ni kujitawala. Neno enkrateia linatokana na neno krat ambalo maana yake ni mamlaka au utawala.   Kiasi ni mojawapo ya tunda la Roho ambalo ni tabia muhimu kwa kila mkristo aliyezaliwa mara ya pili kuwa nalo.   Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa uwezo wa kujitawala na ndio maana ametupa tunda la kiasi. 

Baadhi ya mambo muhimu ambayo  tunayotakiwa kuwa  na tunda la kiasi:
1. Chakula.  Kula kupita kiasi huo ni ulafi. “Husuda, ulevi, ulafi na mambo yanayofanana na hayo….watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” Gal 5:21.
 Mahali pengine tunasoma usile kupita kiasi.  Je umeona asali? Kula kwa kadiri ya kukutosha; usile ukashiba na kuitapika  Mit 25:16.

2. Kuwatembelea wengine.   Mtu anayekwenda nyumbani kwa watu wengine mara kwa mara bila sababu ya maana huyo hana utaratibu. Ndio maana Mungu anatufundisha akisema, “Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi; Asije akakukinai na kukuchukia.” Mit 25:17.

  3. Kutumika katika karama ya Mungu.  Ni muhimu kila mtu kunyenyekea na kutumika katika karama alizojaliwa na Mungu bila kutamani karama za wengine.  Mungu amemngawia kila mmoja karama kama apendavyo yeye. Kila mtu ni kiungo kwa mwenzake na amejaliwa karama tofauti na mwingine, ili mwili wa Kristo ujengwe.  Iwapo mtu amejaliwa kuwa na karama yoyote si mkuu kuliko mwingine bali ni kiungo, ni mjenzi na mtenda kazi katika mwili wa Kristo.  Mtu asije akatamani makuu zaidi kuliko karama aliyojaliwa bali atumike katika karama aliyopewa. Ndio maana imeandikwa;

“....Kila mtu alioko kwenu asinie makuu ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi,kama Mungu alivyomjalia kila mtu kiasi cha imani. Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; hivyo hivyo na sisi tulio viungo wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Basi kwa kuwa tunazo karama zilizo mbalimbali, kwa kadri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake.” Rum 12:3-7.

4. Kuongea kwa kiasi. Ni muhimu kwa mkristo aliyeokoka kuwa makini asiongee  kupita kiasi, bali ayafikiri kwanza atakayoyanena. Kuongea kupita kiasi kumesababisha wengi kujikwaa kwa kusema uongo.  Ni vyema kila mtu kutawala kinywa chake asiwe mwepesi wa kuongea. “Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.” Mit 10:19. “Nalisema, Nitazitunza njia zangu. Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu.” Zab 39;1. “Azuiaye midomo yake ni mwenye maarifa,  Na mwenye roho ya utulivu ana busara” Mit 17:27.

5. Kuwa na kiasi katika kuwaza. Yakupasa kuutawala moyo wako na akili yako bila kuruhusu mawazo mabaya.Ikiwa umejitawala mawazo mabaya hayawezi kupata nafasi. Yakupasa kuwaza mawazo mema kwa kuwa hayo yanampendeza Mungu. Yesu alifundisha akisema; “Ufanyeni mtini kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mtini kuwa mbaya na matunda yake kuwa mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.Enyi wazao  wa nyoka mwawezaje kunena mema? Maana, kinywa cha mtu hunena yaujazayo moyo wake. Mtu mwema  katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.” Mt 12:33-35.

Kutokana na maandiko hayo yanatufundisha tunao uamuzi wa kuamua kuwaza mema au mabaya ambayo ndio yaujazayo moyo wa mtu. Tumepewa tunda la kiasi ili tujitawale na hatimaye kumpendeza Mungu na kusimama imara katika Kristo Yesu.

6. Tamaa mbaya ya mali na fedha. Kuwa na mali na fedha si vibaya bali yakupasa kufanya kazi kwa bidii na kuipata kwa njia za halali kwa kadri Bwana alivyokujalia. Ni muhimu  kuridhika kwa yale ambayo Bwana amekujalia  ili kuepuka  tamaa mbaya ya kumiliki mali na fedha zinazopatiakana   kwa njia za uovu. Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo nanyo; Kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.  Ebr 13:5. “Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tama nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupeda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani na kujichoma kwa maumivu mengi”  Tim 6:9,10. 

Maoni

  1. asante saana ujumbe mzuriiii

    JibuFuta
  2. Hallelujah, l learn something great, l had never seen this message "krat" from today to the rest of my life l w'll put foward "krat" God bless you. Amen.

    JibuFuta
  3. asante nmejifunza kitu

    JibuFuta
  4. Nimejifunza kitu kizuri sana, nimekuwa tu nikiona neno kiasi lakini baada ya kulifuatilia nimegundua lina sehemu kubwa sana kwenye maisha ya mkristo. Mungu akubariki sana kwa utumishi huu.

    JibuFuta
  5. Bila jina12:13

    Nimejifunza namna gani Tunda la kiasi ni la muhimu sana kwenye maisha ya mkristo aliye okoka...Ubarikiwe kwa ufunuo huu.

    JibuFuta
  6. Bila jina10:35

    be blessed

    JibuFuta
  7. Bila jina16:46

    Nimekuelewa sana barikiwa

    JibuFuta
  8. Bila jina12:28

    Asante kwa mafundisho mazuri, Roho Mtakatifu akusaidie zaidi na zaidi kwa mafundisho mengine.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...