Maana ya neno kiasi ni kujitawala.
Neno kiasi linatokana na neno la Kiyunani (enkrateia) ambalo maana yake ni kujitawala. Neno enkrateia linatokana na neno krat ambalo maana yake ni mamlaka au
utawala. Kiasi ni
mojawapo ya tunda la Roho ambalo ni tabia muhimu kwa kila mkristo aliyezaliwa
mara ya pili kuwa nalo. Mungu
alipomuumba mwanadamu alimpa uwezo wa kujitawala na ndio maana ametupa tunda la
kiasi.
Baadhi ya
mambo muhimu ambayo tunayotakiwa
kuwa na tunda la kiasi:
1. Chakula. Kula kupita kiasi huo ni
ulafi. “Husuda,
ulevi, ulafi na mambo yanayofanana na hayo….watendao mambo ya jinsi hiyo
hawataurithi ufalme wa Mungu.” Gal 5:21.
Mahali
pengine tunasoma usile kupita kiasi. Je umeona
asali? Kula kwa kadiri ya kukutosha; usile ukashiba na kuitapika Mit 25:16.
2.
Kuwatembelea wengine. Mtu
anayekwenda nyumbani kwa watu wengine mara kwa mara bila sababu ya maana huyo
hana utaratibu. Ndio maana Mungu anatufundisha akisema, “Mguu wako
usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi; Asije akakukinai na
kukuchukia.” Mit 25:17.
3. Kutumika katika
karama ya Mungu. Ni
muhimu kila mtu kunyenyekea na kutumika
katika karama alizojaliwa na Mungu bila kutamani karama za wengine. Mungu amemngawia kila mmoja
karama kama apendavyo yeye. Kila mtu ni kiungo kwa mwenzake na amejaliwa karama
tofauti na mwingine, ili mwili wa Kristo ujengwe. Iwapo mtu amejaliwa kuwa na
karama yoyote si mkuu kuliko mwingine bali ni kiungo, ni mjenzi na mtenda kazi
katika mwili wa Kristo. Mtu
asije akatamani makuu zaidi kuliko karama aliyojaliwa bali atumike katika
karama aliyopewa. Ndio maana imeandikwa;
“....Kila mtu
alioko kwenu asinie makuu ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi,kama
Mungu alivyomjalia kila mtu kiasi cha imani. Kwa kuwa kama vile katika mwili
mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; hivyo hivyo na
sisi tulio viungo wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa
mwenzake. Basi kwa kuwa tunazo karama zilizo mbalimbali, kwa kadri ya neema
tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo
katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake.” Rum 12:3-7.
4. Kuongea
kwa kiasi. Ni muhimu
kwa mkristo aliyeokoka kuwa makini asiongee kupita
kiasi, bali ayafikiri kwanza atakayoyanena. Kuongea kupita kiasi kumesababisha
wengi kujikwaa kwa kusema uongo. Ni
vyema kila mtu kutawala kinywa chake asiwe mwepesi wa kuongea. “Katika wingi
wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.” Mit 10:19. “Nalisema, Nitazitunza njia
zangu. Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu
mbaya yupo mbele yangu.” Zab 39;1. “Azuiaye midomo yake ni mwenye
maarifa, Na mwenye roho ya
utulivu ana busara” Mit 17:27.
5. Kuwa na
kiasi katika kuwaza. Yakupasa
kuutawala moyo wako na akili yako bila kuruhusu mawazo mabaya.Ikiwa umejitawala
mawazo mabaya hayawezi kupata nafasi. Yakupasa kuwaza mawazo mema kwa kuwa hayo
yanampendeza Mungu. Yesu alifundisha akisema; “Ufanyeni
mtini kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mtini kuwa mbaya na
matunda yake kuwa mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.Enyi
wazao wa nyoka mwawezaje
kunena mema? Maana, kinywa cha mtu hunena yaujazayo moyo wake. Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu
mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.” Mt 12:33-35.
Kutokana na maandiko hayo
yanatufundisha tunao uamuzi wa kuamua kuwaza mema au mabaya ambayo ndio
yaujazayo moyo wa mtu. Tumepewa tunda la kiasi ili tujitawale na hatimaye
kumpendeza Mungu na kusimama imara katika Kristo Yesu.
6. Tamaa
mbaya ya mali na fedha. Kuwa na mali
na fedha si vibaya bali yakupasa kufanya kazi kwa bidii na kuipata kwa njia za
halali kwa kadri Bwana alivyokujalia. Ni muhimu kuridhika kwa yale ambayo Bwana
amekujalia ili kuepuka tamaa mbaya ya kumiliki mali na fedha
zinazopatiakana kwa
njia za uovu. Msiwe na tabia
ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo nanyo; Kwa kuwa yeye mwenyewe
amesema, sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Ebr 13:5. “Lakini hao watakao kuwa na
mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tama nyingi zisizo na maana, zenye
kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la
mabaya ya kila namna ni kupeda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo
wamefarakana na imani na kujichoma kwa maumivu mengi” Tim 6:9,10.
asante saana ujumbe mzuriiii
JibuFutaHallelujah, l learn something great, l had never seen this message "krat" from today to the rest of my life l w'll put foward "krat" God bless you. Amen.
JibuFutaasante nmejifunza kitu
JibuFutaNimejifunza kitu kizuri sana, nimekuwa tu nikiona neno kiasi lakini baada ya kulifuatilia nimegundua lina sehemu kubwa sana kwenye maisha ya mkristo. Mungu akubariki sana kwa utumishi huu.
JibuFutaNimejifunza namna gani Tunda la kiasi ni la muhimu sana kwenye maisha ya mkristo aliye okoka...Ubarikiwe kwa ufunuo huu.
JibuFutabe blessed
JibuFutaNimekuelewa sana barikiwa
JibuFutaAsante kwa mafundisho mazuri, Roho Mtakatifu akusaidie zaidi na zaidi kwa mafundisho mengine.
JibuFuta