Kabla ya kuendele na somo hili tuagalie kwanza maana ya neno pepo.
Neno pepo linamaanisha, pepo mbaya, shetani, mwovu, mharibifu na mwangamizi. Hao ni malaika waliomuasi Mungu wakatupwa duniani. “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na Yule joka (Shetani), Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; Nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, Yule mkubwa, Yule wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufu 12:79.
Neno pepo linamaanisha, pepo mbaya, shetani, mwovu, mharibifu na mwangamizi. Hao ni malaika waliomuasi Mungu wakatupwa duniani. “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na Yule joka (Shetani), Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; Nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, Yule mkubwa, Yule wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufu 12:79.
1. Ili kutoa pepo, kuna
mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa:
Ni lazima uwe na nguvu za Roho
Mtakatifu.Tunaweza kujifunza kwa Yesu alivyoweza kutoa pepo kwa uwezo na nguvu
za Roho. Imeandikwa, “…..awaamuru
pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.” Luka 4:36.
2. Kutoa pepo kwa
jina la Yesu. Aliye na amri
na mamlaka ya kutoa pepo ni mkristo ambaye amemwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na
mwokozi wa maisha yake. “Na ishara
hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo……” Math 16:17. Wale ambao bado hawajamwamini Yesu na
kuokoka, Si vyema kujaribu kutoa Pepo kwa sababu hatatoka, vile vile wanaweza
kushambuliwa na hao walio na Pepo, kama wale wana wa Skewa, Kuhani Mkuu.
“.....wakajaribu kutaja jina la
Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nakuapisha kwa Yesu,
Yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi,
Kuhani Mkuu, walifanya hivyo..... na yule mtu aliye pagawa na pepo wachafu
akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile
hali wa uchi na kujeruhiwa.” Mdo 19:13-16.
3 3. Kufanya maombi kila
siku na wakati mwingine kufunga.
Bila kufanya
hivyo haiwezekani kwa neno lolote, ndio maana Yesu alisema“ Lakini kwa namna hii haitoki ila
kwa kusali na kufunga.” Mat 17:21.
4. Kutoa pepo kwa imani. Unaweza kujifunza kwa wale wanafunzi wa Yesu
waliposhindwa kumtoa pepo Yule kijana. Walishindwa
kwa sababu ya upungufu wa imani. Wangekuwa na imani wangeweza kumtoa Yule pepo. “Kisha wale wanafunzi wakamwendea
Yesu kwa faragha wakisema, mbona sisi hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia kwa
sababu ya upungufu wa imani yenu…..” Mat 17:19-20.
5. Kutoa pepo kwa amri na
mamlaka. Unaamuru kwa
jina la Yesu atoke naye hutoka. Tunaweza kujifunza kwa Mtume Paulo alivyomtoa
pepo Yule kijakazi, akaamuru kwa kumwambia Yule pepo, “..…nakuamuru kwa jina la Yesu
Kristo mtoke huyu, Akamtoka saa ile ile.” Mdo 16:18.
6. Makosa
yanayofanyika kwa wale ambao wanakemea pepo, kwa kuwaambia ninakuangamiza kwa
damu ya Yesu, ninakuteketeza kwa moto, au ninakufunga. Kufanya hivyo ni kinyume
na mamlaka ya Mungu aliyowapa watoto wake. Kwa sababu hiyo, Mungu hajatupa
mamlaka ya kuwaangamiza, Kuwateketeza, wala kuwafunga. Bado pepo watakuwepo
katika dunia hii kwa sababu wakati wao wakuhukumiwa na kuteswa haujafika. Ndio
maana pepo walipomuona Yesu, “…..wakasema,Tuna
nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?” Mat 8:23.
7.Wakati wa kumhudumia
mwenye pepo si sahihi
kuongea na mapepo na kuwaliza maswali wametoka wapi, nani akawatuma, ni kwa nini wanamtesa huyo mtu.
Hatupaswi kumsikiliza shetani na mapepo yake kwa sababu wao ni waovu na waongo siku zote. Ndio maana imeandikwa, “....Asemapo uongo
husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo” Yn 8:44. Yesu Krsto hakufanya hivyo ambaye ndiye
kielelezo chetu katika utumishi, ijapokuwa alimwona yule mtu aliyekuwa
amepagawa na kuteseka siku nyingi alimuuliza swali akitaka kujua jina lake, si
jina la pepo. Badala yake pepo waliokuwa wamemtawala yule mtu walijibu wao ni
jeshi. “Yesu
akamwuliza jina lako nani? Akasema jina langu ni jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia”. LK 8:30.
Pepo atolewapo hutaka kurudi.
Pepo anapotolewa ndani ya mtu aliyempagawa huondoka na
baadae hurudi na kuangalia kama anaweza kuingia tena. Ikiwa mtu huyo anaishi
maisha ya dhambi huona nyumba ni chafu na kuingia."Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali
pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, aspate. Halafu husema, nitarudi
nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara
huenda akachukua pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao
huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya
kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya". Mt12:43-45.
Barikiwe kwa uchambuzi mzuri
JibuFutaBarikiwa Mpakea mafuta wa Bwana
JibuFutaBarikiwa
JibuFuta