Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUTOA PEPO.

Kabla ya kuendele na somo hili tuagalie kwanza maana ya neno pepo.
Neno pepo linamaanisha, pepo mbaya, shetani, mwovu, mharibifu na mwangamizi. Hao ni malaika waliomuasi Mungu wakatupwa duniani. “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na Yule joka (Shetani), Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; Nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, Yule mkubwa, Yule wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufu 12:79. 

1. Ili kutoa pepo, kuna mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa:
        Ni lazima uwe na nguvu za Roho Mtakatifu.Tunaweza kujifunza kwa Yesu alivyoweza kutoa pepo kwa uwezo na nguvu za Roho. Imeandikwa, “…..awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.” Luka 4:36. 
        
     2. Kutoa pepo kwa jina la Yesu. Aliye na amri na mamlaka ya kutoa pepo ni mkristo ambaye amemwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake. “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo……” Math 16:17. Wale ambao bado hawajamwamini Yesu na kuokoka, Si vyema kujaribu kutoa Pepo kwa sababu hatatoka, vile vile wanaweza kushambuliwa na hao walio na Pepo, kama wale wana wa Skewa,  Kuhani Mkuu.

“.....wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nakuapisha kwa Yesu, Yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, Kuhani Mkuu, walifanya hivyo..... na yule mtu aliye pagawa na pepo wachafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.”  Mdo 19:13-16.

3 3. Kufanya maombi kila siku na wakati mwingine kufunga. 
Bila kufanya hivyo haiwezekani kwa neno lolote, ndio maana Yesu alisema Lakini kwa namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.” Mat 17:21.
     
     4. Kutoa pepo kwa imani. Unaweza kujifunza kwa wale wanafunzi wa Yesu waliposhindwa kumtoa pepo Yule kijana. Walishindwa kwa sababu ya upungufu wa imani. Wangekuwa na imani wangeweza kumtoa Yule pepo. “Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakisema, mbona sisi hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia kwa sababu ya upungufu wa imani yenu…..” Mat 17:19-20.
    
      5. Kutoa pepo kwa amri na mamlaka. Unaamuru kwa jina la Yesu atoke naye hutoka. Tunaweza kujifunza kwa Mtume Paulo alivyomtoa pepo Yule kijakazi, akaamuru kwa kumwambia Yule pepo, “..…nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo mtoke huyu, Akamtoka saa ile ile.” Mdo 16:18.

6. Makosa yanayofanyika kwa wale ambao wanakemea pepo, kwa kuwaambia ninakuangamiza kwa damu ya Yesu, ninakuteketeza kwa moto, au ninakufunga. Kufanya hivyo ni kinyume na mamlaka ya Mungu aliyowapa watoto wake. Kwa sababu hiyo, Mungu hajatupa mamlaka ya kuwaangamiza, Kuwateketeza, wala kuwafunga. Bado pepo watakuwepo katika dunia hii kwa sababu wakati wao wakuhukumiwa na kuteswa haujafika. Ndio maana pepo walipomuona Yesu, “…..wakasema,Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?” Mat 8:23.

7.Wakati wa kumhudumia mwenye  pepo si sahihi kuongea na mapepo na kuwaliza maswali wametoka wapi, nani akawatuma, ni  kwa nini wanamtesa huyo mtu. Hatupaswi kumsikiliza shetani na mapepo yake kwa sababu wao ni waovu  na waongo siku zote. Ndio maana imeandikwa, “....Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo”  Yn 8:44. Yesu Krsto hakufanya hivyo ambaye ndiye kielelezo chetu katika utumishi, ijapokuwa alimwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na kuteseka siku nyingi alimuuliza swali akitaka kujua jina lake, si jina la pepo. Badala yake pepo waliokuwa wamemtawala yule mtu walijibu wao ni jeshi. “Yesu akamwuliza jina lako nani? Akasema jina langu ni jeshi;  kwa sababu pepo wengi wamemwingia”. LK 8:30. 

Pepo atolewapo hutaka kurudi. 
 Pepo anapotolewa ndani ya mtu aliyempagawa huondoka na baadae hurudi na kuangalia kama anaweza kuingia tena. Ikiwa mtu huyo  anaishi maisha ya dhambi huona nyumba ni chafu na kuingia."Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, aspate. Halafu husema, nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda akachukua pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya". Mt12:43-45. 

Maoni

  1. Barikiwe kwa uchambuzi mzuri

    JibuFuta
  2. Bila jina20:14

    Barikiwa Mpakea mafuta wa Bwana

    JibuFuta
  3. Bila jina11:34

    Barikiwa

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...