Kuishi kwa amani ni jambo la muhimu sana katika maisha yako, ikiwa umekwisha kumpokea Yesu Kristo na Roho mtakatifu. Utaweza kuamua mambo mbalimbali kwa kumwomba Mungu akupe ufumbuzi. Neno la Mungu linasema; “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu...” Kol 3:15. Hapa ninatoa ushuhuda wangu, katika maisha yangu nimekutana na mambo magumu yanayohitaji maamuzi. Lakini kwa kuwa nilimwomba Bwana hakukawia, alinijalia kuwa na wazo la uamuzi wa kutoa, na ndani ya moyo wangu nilikuwa na amani. Na yote niliyoyatolea maamuzi yalikuwa ni sahihi sawasawa na mwongozo wa Mungu.
Kufanya kazi kwa haki.
Kama wewe ni mwalimu, daktari, kiongozi, mfanyabiashara, askari au unafanya kazi yoyote inakupasa kuifanya kwa haki. Kwa kufanya hivyo ndipo utakuwa na amani na utulivu moyoni mwako; na pia utakuwa na haki ya kumtumaini Mungu kama ilivyoandikwa, “Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa utulivu na matumaini daima” Isa 32:17. Kama hutendi haki huwezi kuwa na amani na utulivu na matumaini mbele za Mungu, ndiyo maana imeandikwa; “Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka. Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu” Isa 57:20, 21. Mwanadamu anapoishi hapa duniani hawezi akapata amani kutokana na vitu alivyonavyo kwa wingi kama fedha, dhahabu, magari, nyumba, mashamba na viwanja. Kwa hiyo amani inapatikana kwa Mungu na Yesu . Ndio maana imeandikwa. “... na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Bwana wetu” 2Tim 1:2. “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na iwe amani kwa watu aliowaridhia” (aliowakubali) Lk 2:14.

Mwisho wa mweye haki ni amani.
Mtu ambaye amezingatia na kudumu katika amani ya Mungu anafikia mwisho kwa amani."Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu,Maana mwisho wa mtu huyo ni amani” Zab 36:37. Tumwangalia Stefano ni mfano mzuri wa kufuata kwa sababu alikuwa ni mkamilifu na mnyofu. Alipopigwa kwa mawe kabla ya kufa aliwasamehe wauaji akafa katika amani. Imeandikwa; “Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu pokea roho yangu. Akipiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana uwasamehe dhambi hii. Akiisha sema hayo akalala..” Mdo7: 59-60. Pia Bwana wetu Yesu Kristo alipoteswa na kusulubiwa aliwasamehe wauaji akafa katika amani. “Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la kichwa, ndipo walipomsulibisha... Yesu akasema, Baba, uwasamehe,...” Lk23:33-34. Ili kufikia mwisho katika amani ni lazima kudumu katika haki na kuepuka dhambi.
Mtu yeyote akikosewa kama hamsamehi aliyemkosea kila akikutana naye hawezi kuwa na amani. Lakini akimsamehe atakuwa na amani. Kumsamehe aliyekukosea ni kutimiza sheria ya Mungu kama ilivyoandikwa, “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu” Mt6:14-15. Mungu anataka ukae kwa amani na watu wote na kudumu katika utakatifu ili uweze kumwona yeye. Kwa sababu hiyo imeandikwa,“Kama kwa yamkini, kwa wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; imeendikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa,asema Bwana” Rum12:18-19. “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo” Ebr12:14-15.
ameni imenibariki
JibuFutaNatamani kupata kitabu
JibuFutaBarikiwa
JibuFuta