Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUISHI KATIKA AMANI.


Kuishi kwa amani ni jambo la muhimu sana katika maisha yako, ikiwa umekwisha kumpokea Yesu Kristo na Roho mtakatifu. Utaweza kuamua mambo mbalimbali kwa kumwomba Mungu akupe  ufumbuzi. Neno la Mungu linasema; “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu...” Kol 3:15. Hapa ninatoa ushuhuda wangu, katika maisha yangu nimekutana na mambo magumu yanayohitaji maamuzi. Lakini kwa kuwa nilimwomba Bwana hakukawia, alinijalia kuwa na wazo  la uamuzi wa kutoa, na ndani ya moyo wangu nilikuwa na amani. Na yote niliyoyatolea maamuzi yalikuwa ni sahihi sawasawa na mwongozo wa Mungu.

Kufanya kazi kwa haki. 
Kama wewe ni mwalimu, daktari, kiongozi, mfanyabiashara, askari au unafanya kazi yoyote inakupasa kuifanya  kwa haki. Kwa kufanya hivyo ndipo utakuwa na amani na utulivu moyoni mwako; na pia utakuwa na haki ya kumtumaini Mungu kama ilivyoandikwa, “Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa utulivu na matumaini daima” Isa 32:17. Kama hutendi haki huwezi kuwa na amani na utulivu na matumaini mbele za Mungu, ndiyo  maana  imeandikwa; “Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka. Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu”  Isa 57:20, 21.                                                                                                Mwanadamu anapoishi hapa duniani hawezi akapata amani kutokana na vitu alivyonavyo kwa wingi kama fedha, dhahabu, magari, nyumba, mashamba na viwanja. Kwa hiyo amani inapatikana kwa Mungu na Yesu . Ndio maana imeandikwa. “... na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Bwana wetu” 2Tim 1:2.  “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na iwe amani kwa watu aliowaridhia” (aliowakubali) Lk 2:14. 

Mwisho wa mweye haki ni amani. 
Mtu ambaye amezingatia na  kudumu katika amani ya Mungu anafikia mwisho kwa amani."Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu,Maana mwisho wa mtu huyo ni  amani” Zab 36:37. Tumwangalia Stefano ni mfano mzuri wa kufuata kwa sababu alikuwa ni mkamilifu na mnyofu. Alipopigwa kwa mawe kabla ya kufa aliwasamehe wauaji akafa katika amani. Imeandikwa; “Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu pokea roho yangu. Akipiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana uwasamehe dhambi hii. Akiisha sema hayo akalala..” Mdo7: 59-60. Pia Bwana wetu Yesu Kristo alipoteswa na kusulubiwa aliwasamehe wauaji akafa katika amani. “Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la kichwa, ndipo walipomsulibisha... Yesu akasema, Baba, uwasamehe,...”  Lk23:33-34. Ili kufikia mwisho katika amani ni lazima kudumu katika haki na kuepuka dhambi.

Mtu yeyote  akikosewa kama hamsamehi aliyemkosea kila akikutana naye hawezi kuwa na amani. Lakini akimsamehe atakuwa na amani. Kumsamehe aliyekukosea ni kutimiza sheria ya Mungu kama ilivyoandikwa, Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu” Mt6:14-15Mungu anataka ukae kwa amani na watu wote na kudumu katika utakatifu ili uweze kumwona yeye. Kwa sababu hiyo imeandikwa,“Kama kwa yamkini, kwa wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; imeendikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa,asema Bwana” Rum12:18-19. “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo” Ebr12:14-15.

Maoni

  1. Bila jina09:29

    ameni imenibariki

    JibuFuta
  2. Bila jina18:45

    Natamani kupata kitabu

    JibuFuta
  3. Bila jina03:26

    Barikiwa

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...