Ruka hadi kwenye maudhui makuu

VIFO VYA MITUME WA YESU.


Mathayo-Alikufa kwa kuuwawa kwa upanga mbali kidogo na mji wa Ethopia.

Marko  - Alikufa kule Alexandria baada ya kukokotwa kikatili kwenye barabara ya mji.

Luka - Alitundikwa juu ya mti wa mizeituni katika nchi ya Kigiriki ya kimaendeleo.

Yohana - Alitiwa kwenye pipa la mafuta yanayochemka lakini hakufa kwa njia ya miujiza na baadaye akapelekwa kwenye  Kisiwa cha Patimo ili afe hata hivyo hakufa huko. Alikufa huko Efeso miaka 100 BK.

Petro  Alisulubiwa kule Rumi kichwa chini miguu juu mwaka 67 BK.

Yakobo Zebedayo  Alikatwa kichwa kule Yerusalemu mwaka 44 BK, Mdo 12:1-2.

Yakobo wa Alifayo  Alitupwa kutoka kwenywe kinara na kisha kupigwa na rungu lenye  misumari mpaka kufa, mwaka 62 BK.

Batholomayo  Alichunwa ngozi akiwa hai mpaka akafa.

Andrea  Alifungwa kwenye msalaba huku akiendelea kuwahubiria wale watesi wake  mpaka kufa.

Thomaso  Alishindiliwa mkuki ndani ya mwili kule Klemandel nchi ya India ya mashariki.
                      
Yuda Thadayo  Alipigwa kwa mkuki mpaka akafa.

 Barnaba wa Mataifa  Alipigwa kwa mawe kule Thesolonike.

Mathayo  Kwanza alipigwa kwa muda mrefu na baadaye akakatwa kichwa.

Paulo  Aliteswa kwa muda mrefu na baadaye kukatwa kichwa kule Rumi na Mfalme Nero mwaka 67 BK.

Historia hii ya vifo vya Mitume aliiandika Dk. Mulu Bale wa Ikizu store – Kororogwa Kibaha. Aliinukuu kwenye kitabu kinachoitwa NIGHTSMATER BOOK OF ILLUSTRATIONS.   

Maoni

  1. Asante sana kwa kutafuta taarifa hii inayohusu vifo vya mitume.

    JibuFuta
  2. Mbona hawakuweka myaka walio kufa

    JibuFuta
  3. Bila jina22:40

    Yesu akubariki mtumishi

    JibuFuta
  4. Bila jina18:47

    Amen

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...