Mungu alituumba kwa kusudi la kuishi katika maadili ya neno lake, ndio maana imeandikwa, “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo” Waefeso 2:10. Mavazi ya mwanamke Neno lake Mungu linatufundisha maadili ya mavazi ya kuvaa kwa mwanamke. Vivyo hivyo wanawake wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri…" 1Timotheo 2:9. Ikiwa mwanamke amevaa gauni fupi, linalobana au lililopasuli na kuonyesha sehemu zake za mwili ambazo hazipaswi kuonekana wazi anajiabisha na kujivunjia heshima mbele za Mungu na jamii. Kujichubua uso ni kuondoa rangi ya asili aliyoumbwa nayo. Kunyoa nyusi na kupaka rangi badala ya nyusi na kuvaa nywele badia, haya si maadili ya neno la Mungu. Mwanamke afanyaye mambo kama haya hapa juu anampinga na kumkosoa muumbaji wake ambaye ni Mungu. Ni sawa na kumwambia alikosea alivyomu...
Blogu hii imekuwa msaada kwa watu wengi. Wamelifahamu neno la Mungu na kuimarika katika kumjua Mungu. Washirikishe na wengine.