Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UBATIZO.

Maana ya neno ubatizo.
Neno ubatizo linatokana na neno la Kiyunani baptizo. Maana ya neno baptizo ni kuzamisha.                  

Kubatizwa ni agizo la Mungu.  
Mungu alimtuma Yohana aje duniani kuhubiria watu watubu dhambi zao na kuwabatiza. “Tubuni, kwa maana  ufalme wa Mungu umekaribia” Mathayo 3:2. “Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordan; Naye akawabatiza katika mto Yordani, huku wakiziungama dhambi zao” Mathayo 3:5,6.

Asiyeye kubali kabatizwa atahukumiwa.    
Kubatizwa ni mojawapo ya sheria za Mungu ambazo mwanadamu anapaswa kuzitii. Asiye kubali kubatizwa hataingia katika ufalme wa Mungu. “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa” Marko 16:16.

Kubatizwa katika maji mengi.   
Hii ni sheria ya Mungu  yakuzingatia kama vile Yesu Kristo alivyo batizwa katika maji mengi. “Naye Yesu alipokwisha batizwa mara akapanda kutoka majini” .…Mathayo 3:16. Yesu alisisitiza ni lazima Mtu azaliwe kwa maji. Ukweli ili Mtu azaliwe kwa maji ni lazima azamishwe ndani ya maji, anapopanda kutoka majini anakuwa amezaliwa kwa maji. “Yesu akajibu amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji….. hawezi kuingia ufalme wa Mungu” Yohana 3:5. “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa” Yohana 3:23.   
 Sababu ya kubatizwa:
1. Ni kutimiza haki au sheria ya Mungu, ndio maana Yesu alimwendea Yohana ili abatizwe. “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe,nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo (sisi) kuitimiza haki yote. Basi akamkubali” Mathayo 3:13 -15.

2. Ni ishara ya kuzikwa pamoja na Kristo katika mauti yake. “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?.  Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake”…..Warumi 6:3,4.                                                          
Ubatizo wa toba.    
Wakati Yohana akibatiza watu walipomwendea waliziungama dhambi zao na kubatizwa, ndio maana ukaitwa ubatizo wa toba kwa sabhabu mambo haya mawili yalifanyika kwa wakati mmoja ijapokuwa kila moja linajitegemea na lina maana yake. Kubatizwa hakuondoi dhambi bali ni kuitimiza haki au sheria ya Mungu. Toba ni neno linalomaanisha kuungama dhambi mbele za Mungu. Dhambi huondolewa na Mungu mtu anapoungama. “Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” 1Yohana 1:9  

Ni nani anayebatizwa?
Ni Mtu mzima kwa sababu anaweza kufahamu neno la Mungu na kuliamini ndio maana imeandikwa “aaminiye” pia anaweza kuwa na “dhamiri  safi” neno dhamiri limaanisha nia “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa” Marko 16:16. “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo” 1Petro 3:21.

Watoto wadogo hawabatizwi.
Kwa sababu bado ni wadogo hawawezi kuamini, hawajafikia kuwa watu wazima. Katika sheria ya Mungu kwenye Biblia hakuna mahali popote imeandikwa watoto walibatizwa, bali walibarikiwa. “Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu  ni wao. Amini, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama watoto wadogo hataingia kabisa. Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabarikia” Marko 10:13-16.    

Usipunguze wala kuongeza kuhusu ubatizo.     
Kwa sababu Mungu ameagiza kubatizwa kwa maji mengi yatupasa kufanya hivyo na sii vinginevyo. Yatupasa kumtii Mungu kwa sheria zake zote bila kuzipindisha au kwenda kinyume nazo. Kwa mfano wewe una mtoto wako umempa agizo aoge lakini yeye kwa utashi wake akaamua kunawa miguu je, ametimiza agizo lako? endelea kufikiri je, utafurahi kwa kitendo chake kwa kufanya kinyume na agizo lako?

Anayeongeza au kupunguza maagizo au maneno ya Mungu hataingia kwenye uzima wa milele mbinguni. “Na mtu akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki”. Ufunuo 22:19. “Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguza, mpate kuzishika  amri za Bwana,  Mungu wenu, niwaamuruzo” Kumbukumbu 4:2.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...