Kutokusamehe wengine
Kitendo cha kutosamehe wanaokukosea ni dhambi kama dhambi
zingine . Kusamehe ni agizo la Mungu na ni wajibu wako. “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa
yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa
yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu” Mathayo 6:14,15. Unapokosewa usingoje kuombwa msamaha
unapaswa kumsamehe aliyekukosea kwa wakati huo huo.
Unapomsamehe aliyekukosea unakuwa na amani na utulivu ndani ya
moyo wako na ndio maana imeandikwa, “ Linda moyo wako kuliko yote
uyalindayo;-------” Mithali 4:23.Unapolinda moyo wako unakuwa salama. Ili
kuendelea kuwa salama yakupasa uepuke ugomvi, mabishano na maneno
yasiyofaa,
hayo hayana maana huleta uharibifu katika moyo wako.
Maneno yasiyo maana
Kwa maadili ya Mungu ametuumba kwa ajili ya mema katika kutenda na
kusema.
Anataka tumpendeze yeye katika mambo yote, na ndipo tutaurithi
ufalme wa Mungu.
Maneno yasiyo maana ni kama, kutaniana, kudhihaki, matusi, ugomvi,
mabishano na yanayofanana na hayo. “Msidanganyike mazungumzo mabaya
huharibu tabia njema” 1Wakorintho 15:33. “Basi, nawaambia, kila neno lisilo
maana,watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa
kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa” Mathayo 12:36,37.
Kujisifu
Mungu ametuonya na kutufundisha tusijisifu kwa mambo yoyote
kwa kuwa hapendezwi na hayo. “Bwana asema hivi, mwenye hekima asijisifu
kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu
zake,wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; bali ajisifuye ajisifu
kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi,na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana,
nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo
hayo, asema Bwana” Yeremia 9:23,24.
“Haya basi, ninyi msemao, leo au kesho
tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na
kupata faida; walakini hujui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana
ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha kutoweka. Badala ya kusema Bwana
akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi. Lakini sasa mwajivuna katika
majivuno yenu, kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya” Yakobo 4:13-16. “Msitende neno lo lote kwa kushindana
wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mweziwe kuwa bora
kuliko nafsi yake” Wafilipi 2:3.
Kiburi
Wenye kiburi watahukumiwa, ni vizuri kujichunguza katika maisha
yako usije ukahukumiwa. “Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo
kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu. Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho ya
kutakabari hutangulia maanguko” Mithali 16:5,18.
Hasira
Sii vyema kukasirika kwa kuwa utatenda isivyo haki, ili kujilinda
na kuwa salama wakati wowote, unapokosewa samehe, nawe utakuwa na amani na
utulivu. Katika maisha yako kamwe usiruhusu kukasirika kwa sababu
kutakusababishia uchungu na kufadhaika moyoni mwako. Unapokosewa ni vema
kutawala moyo wako usiwe na haraka ya kusema, imeandikwa hivi, “Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa;
Na mwenye roho ya utulivu ana busara” Mithali 17:27. “Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko
shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji” Mithali 16:32.
Maoni
Chapisha Maoni