Mwendelezo wa somo la maombi lililotangulia.
Karibu endelea kujifunza.
5. Kuomba kwa bidii bila kukata tamaa.
Maombi ya namna hii ni dua, unamwomba Mungu tena na tena hadi
anakupa unachokihitaji. Ukisoma habari za Watumishi wa Mungu walifanya maombi
ya dua na kupokea waliyoyahitaji. Na si hivyo tu, Bwana wetu Yesu Kristo
alifanya dua na kutufundisha kuomba kwa bidii na kupokea. “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea
yule, awezaye kumwokoa kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana
na machozi,akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu” Waebrania 5:7.
“Akawaambia mfano, imewapasa kumwomba Mungu
siku zote, wala wasikate tamaa, Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani,
hamchi Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane,
aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda
alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu na kujali watu,
lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha
kwa kunijia daima. Bwana akasema, sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. Na
Mungu je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni
mvumilivu kwao? Nawaambia atawapatia haki upesi…" Luka 18:1-8.
"… Naye
Eliya akapanda juu mpaka kilima cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso
mpaka magotini. Akamwambia mtumishi wake, kwea sasa, utazame upande wa
baharini. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu. Naye akasema, enenda tena
mara saba. Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari,
nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika ushuke
mvua isikuzuie. Ikawa muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo,
ikanya mvua nyingi…" 1Wafalme 18:42- 45. Haya maaandiko yanaonyesha jnsi Eliya alivyomwomba Mungu
mara sita mvua haikunyesha, lakini hakukata tamaa aliomba tena kwa mara
ya saba na mvua ikanyesha. Hakika Mungu anajibu maombi ukiomba kwa bidii.
6. Jinsi ya kuomba
1) Kuomba kwa jina la Yesu.
“Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo
nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina
langu, nitalifanya” Yohana 14:13, 14.
2) Kwa mfano maombi ya ulinzi. Ee Mungu Baba kwa jina la Yesu, ninakuomba unilinde salama, na kuniepusha na hatari zote. Ninakushukru kwa kuwa umenisikia ni katika jina la Yesu. Amen.
7.Kuomba na kushukuru.
“ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila
jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu” 1Wathesalonike 5:17,18. “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika
kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushuru, haja zote na zijulikane na
Mungu” Wafilipi 4:6.
8. Kabla ya
kumwomba Mungu hujibu.
Ahadi hii inawezekana kwa wale
waliomwamini Mungu na kupokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wao.“Naitakuwa ya
kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na
wakiwa katika kunena nitasikia” Isaya 64:24. “...maana Baba yenu anajua mnayohitaji
kabla ninyi hamjamwomba” Mathayot 6:8. “Umtumaini Bwana ukatende
mema,...Nawe utajifurahisha kwa Bwana, Naye atakupa haja ya moyo wako”. Wakati
mwingine hata kabla ya kuomba unapewa haja ya moyo wako, lakini kwa kutimiza
agizo la kumtumaini (kumtegemea) na kutenda mema.
Kujibiwa kabla ya kuomba ni kwa neema yake Mungu katika Kristo
Yesu. Haimaanishi tusiombe, yatupasa kuomba ni wajibu wetu kwa kuwa yeye hujibu
maombi kwa kulitukuza jina lake katika Yesu
Kristo. “Mkiomba neno
lo lote kwa jina langu hilo nitalifanya ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana” Yohana
14:13. Mungu
hufanya zaidi ya yale tuyaombayo na kuyawaza.“Basi atukuzwe
awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa
kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu” Waefeso
3:20.
Sababu za kuomba.
) Kuomba tusiingie majaribuni “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi lakini
mwili ni dhaifu” Mathayo 26:41.
) Kuomba kwa ajili mahitaji yetu
mbele za Mungu.
Wakati wa kuomba
Kila wakati. “Kwa sala zote na maombi mkisali kila
wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu kuwaombea watakatifu
wote” Waefeso 6:18. “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika
kuomba huku na shukrani” Wakolosai 4:2.
Mahali pa kufanyia maombi
1. Hekaluni (Kanisani). “Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea
pamoja kwenda hekaluni saa ya kusali, saa tisa” Matendo 3:1.
2. Chumbani. “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba
chako cha ndani, na ukiisha funga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye
sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi” Mathayo 6:6.
3.Mahali
panapofaa.
Yesu alikwenda katika mlima Mizeituni na wanafunzi wake kuomba. “Akatoka akaenda mlima Mizeituni kama
ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake wakafuatana naye. Alipofika mahali pale
aliwaambia ombeni… Mwenyewe akajitenga nao…akapiga magoti akaomba” Luka 22:39- 41. Paulo na sila walikuwa wanatafuta mahali
pa faragha wakasema hivi “… tukaenda kando ya mto, Ambapo tukadhani
yakuwa pana mahali pa kusali…" Matendo 16:13.
Sababu maombi kutojibiwa
1. Kuishi maisha ya dhambi.
“Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi…” Yohana 9:31.
“Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka hata
asiweze kuokoa; wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu
yenu yamewafarakanisha ninyi na Mungu wenu,na dhambi zenu zimeuficha uso wake
msiuone, hata hataki kusikia” Isaya 59:1,2.
2. Komba pasipo na imani
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; naye akisita-sita,
Roho yangu haina furaha naye “Bwana akasema, kama mngekuwa na imani kiasi
cha chembe ya haradali, mgeuambia mkuyu huu, Ng’oka, nao ukapandwe baharini,
nao ungewatii” Luka 17:6. “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;
kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa
thawabu wale wamtafutao” Waebrania 10:38, 11:6.
Maoni
Chapisha Maoni