KULEA WATOTO WADOGO KATIKA MAADILI MEMA
Mzazi au mlezi yampasa kufahamu ya kwamba yeye kama Mwalimu na mfano wa kuigwa katika familia yake. Kwa kawaida watoto hujifunza mambo wanayoyaona au kusikia kwa wazazi, walezi, Waalimu na watu wengine. Kwa hiyo watoto kuwa na maadili mema au mabaya ni kutokana na malezi ya pande zote. Kwa kawaida watoto walivyo bado hawajaweza kupambanua yaliyo mema na mabaya. Lakini wakielimishwa yaliyo mema na mabaya ni yapi!
Kuna mambo muhimu ambayo mtoto anapaswa kufundishwa katika haya maneno:
1.Kumfundisha mtoto kusema neno asante. Neno asante ni muhimu kwa kila mtu apewapo kitu au kutendwa jambo lolote jema. Kwa hiyo yampasa kusema neno asante. Kwa kufanya hivyo ni jambo jema na pia maadili kwa watu wa rika zote.
Kama mtu hatoi shukrani kwa yale mema ambayo ametendewa huenda yamkini hakulelewa tangu akiwa mtoto ya kwamba yampasa akipewa chakula au amemnunulia nguo aseme asante, au anapopewa kitu chochote na wazazi wake. Usipomlea mtoto katika maadali mema atakapokuwa mtu mzima hataona umuhimu wa kushukuru. Ndio maana kuna baadhi ya watu kusema neno la shukrani. Ndio maana kuna mithali inasema umleavyo mtoto ndivyo akuavyo. Kutokana na msemo huo unadhihirisha mambo mawili.
Jambo la kwanza na msingi ni mzazi au mlezi kumlea mtoto katika maadili mema. Kwa hiyo atakua maadili. Kwa hiyo katika maisha yake yote ataishi katika maadili mema, ndio maana neno linasema “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” Mithali 22:6 Lakini ikiwa ni hatalelewa katika maadili yanayofaa kuwa na maadili mema katika maisha yake. Kwa hiyo ni muhimu kwa wazazi au walezi kuwa makini na kuwasaida ili baadae nao waweze kuwa wazazi maadili mema. 2. Kumfundisha mtoto maneno ya Mungu na jinsi ya kumwabudu Mungu kwa kufanya maombi, kutoa sadaka, kumsifu na kumwabudu Mungu.
3. Kumfundisha kuwa mkarimu. Ni wakati umempa biskuti au karanga na kumwambia amgawie mtu mwingine. Ikiwa hatafanya hivyo endelea kumzoesha kwa kuchukua ulichompa kama ni karanga na kumgawia mtu mwingine halafu mbakizie zake . Kwa kufanya hivyo unakuwa umemfundisha kuwa mkarimu. Kwa hiyo siku nyingine akipewa karanga anaweza kumngawia mtoto mwenzake au mtu mwingine. Hiyo ndiyo njia sahihi ya kuondoa ubinafsi na uchoyo ndani ya nafsi ya mtoto.
Jambo lingine mzazi au mlezi
jikoni jikoni anapika chakula ni muhimu awe makini asije akawa anampa mtoto chakula au jikoni jikoni. Nasema hivyo kwa sababu mtoto anapoona chakula anachokipenda sana anaweza akalilia na kuomba apewe. Kama utakuwa unampa kidogo jikoni kabla ya chakula mezani kwa ajili ya kuwa na watu wote, utakuwa unamjenga mtoto kuwa na tabia ya ubinafsi na uchoyo. Mpishi anapokuwa amepika chakula halafu mtoto anachukue kinyango cha nyama au kipande cha Chipsi katika sufuria na kukila. Ukiona mtoto amefanya hivyo na wewe unamwacha kwa kusema moyoni kwa kuwa ni mtoto mdogo tu, atakua na kuacha. Ukisema hivyo sio sahihi kwa sababu hiyo ni tabia ambayo mtoto ameanza ya udokozi, ijapokuwa anachukua wakati unamwona. Kwa hiyo yakupasa kumkataza kumwambia asubiri mpaka chakula mezani naye atapewa. Kuna baadhi ya wapishi wenye uchu wa nyama au chakula wanachokipenda wakati wanapopika wanakula kwa kiasi fulani jikoni jikoni. Mtu wa namna hiyo ni mlafi hawezi kurithi ufalme wa Mungu. “...ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” Wagalatia 5:21.
4. Kumfundisha mtoto kula kwa kiasi. Ikiwa kuna chakula anachokipenda sana mpe kwa kiasi cha kushiba. Baada ya kula akiomba kuongezewa chakula mwongezee kidogo sana, au mwambie ulichokula kinatosha. Watoto wadogo huwa wanaelewa wakielekezwa.
Lakini yakupasa kuchuliana na mtoto kwa uvumilivu usiwe mwepesi wa hasira kutokana na mambo ambayo analilia. Fahamu ya kwamba kwa kawaida ya watoto ili wapate yale wanayoyahitaji ni kwa njia ya kulia. Ikiwa mtoto mdogo ana njaa, kiu, usingizi, maumivu makali, ameachwa na mama yake mwenyewe au kuna kitu anataka apewe. Wakati mwingine kuna kitu amesogelea hajaweza kukifikia. Kutokana na sababu hizo mtoto hulia.
5. Kumfundisha mtoto Kuwa na nidhamu. Awe anaamkia watu ambao ni wakubwa kwake kwa umri. Asiwazoe wageni wanaokutembelea nyumba kwako na hatimaye kuwasumbua.
Kwa hiyo ili kuwa na taifa lenye maadili mema ni lazima mtoto ajengwa maadili mema nyumbani. Kwa hiyo sio sahihi kuwaacha watoto kuangalia picha katika televisheni na intaneti ambazo sio salama kwa watoto, zinaharibu maadili ya watoto. Pia kuna baadhi ya machapisho ambayo yana picha na maneno yasiyo salama kwa watoto. Kwa hiyo yakupasa kumlinda na kumwelisha mtoto wako kwa kumweleza ni yapi yanafaa na yasiyofaa. Jambo lingine la muhimu yakupasa kutambua kuhusu mtoto wako rafiki zake ni nani! Ili kuchunguza na kubaini tabia za hao rafiki zake, Je? Ni nzuri au mbaya. Njia ya kutumia ni kupitia mtoto mwenyewe kwa kuwa na ukaribu naye kwa maongezi. Kwa mfano unaweza ukauliza rafiki zake ni nani! hata kama unawafahamu. Kwa hiyo anaweza kukuambia habari za watoto wenzake na hata rafiki zake. Kwa hiyo unaweza kufahamu marafiki zake na watoto wengine. Kama atakuwa ameeleza tabia za watoto ambazo ni kinyume na maadili mema mshauri kwa kumwambia hayo wanayoyafanya sio maadili mema. Pia mkataze asije akayaiga hayo. Vilevile mwepumshe mtoto wako na marafiki wabaya. Kwa kufanya hivyo utakuwa umemjenga katika maadili mema.
Maoni
Chapisha Maoni